KAMATI YA UTENDAJI SIMBA YATEUA WAJUMBE WA KAMATI 3 TOFAUTI

MWANACHAMA maarufu wa Simba Zakaria Hans Pope ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, sambamba na kuteuliwa na mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji.


Aizungumza jijini Dar es Salaam jana mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alisema kamati ya utendaji iliyokutana juzi ambapo ilijadili taarifa ya makabidhiano na kuteua viongozi wa kamati za Usajili,fedha na mashindano.

Alisema kamati ilimteua pia Kassim Dewji kuwa mshauri mkuu wa kamati ya usajili huku Geofrey Iriki Nyange ‘Kaburu’akiteuliwa kuwa makamu mwenyekiti, Mulamu Ng’ambi aliteuliwa kuwa Katibu na wajumbe ni Azim Dewji, Patric Paul, Salim Abdala na Musley Ruhey.


Rage alisema kamati ya fedha itaongozwa na Kaburu (Mwenyekiti), Joseph Itang’re Kinesi (Makamu Mwenyekiti), Onesmo Waziri (Katibu), huku wajumbe ni Said Pamba, Eubert Mhanda, Johnson Masasawa na Andrew Tupa.

Wakati kamati ya mashindano itakuwa chini Hassan Othman ‘Hassanoo’ (Mwenyekiti), Danny Manembe (makamu mwenyekiti), Adam Mgoi, Jerry Yambi, Seleman Zakazaka, Hassan Bantu na Gerald Lukumai

Comments