KAMATI MISS TZ YAIVULIA KOFIA MISS TABATA 2010

WASHIRIKI MISS TABATA 2010

Mkurugenzi wa Miss Tanzania Hashim Lundenga juzi alivutiwa na maandalizi ya warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambao limepangwa kufanyika Ijumaa katika Ukumbi wa Dar West Park , Tabata.


Lundenga alisema wengi wa warembo hao wanasifa ya kushinda taji la Vodacom Miss Tanzania iwapo watajiamini na kutofuata tabia mbaya zinazofanywa na baadhi ya warembo waliyowahi kushiriki kwenye mashindano hayo.

Lundenga alisema hayo wakati alipotembelea kambi ya warembo wanaoshiriki Miss Tabata Jumapili katika ukumbi wa Dar West Park ambapo alisema kamati yake ni safi lakini tabia chafu zinazofanywa na baadhi ya warembo waliyowahi kushinda mataji mbali mbali zinafanya kamati yake ionekane haifai.

“Sisi tunaka na nyinyi siku 30 tu ambazo ni chache mno kutufanya tujue tabia zenu. Warembo wengi huwa wanaficha tabia zao wanaposhiriki lakini baada ya kushinda huwa huonyesha tabia zao mbaya kwa jamii,” Lundenga aliwaambia warembo hao.

“Tumegundua kuwa warembo wengi huwa nanapakaziwa na huonewa lakini hawana tabia mbaya,” mkurugenzi huyo alisema.

Warembo watakaoshiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo litafanyika Ijumaa katika ukumbi wa Dar West, Tabata ni Ritha Swai (19), Upendo Paul (18), Jesca Mariwa (19), Ummy Mohamed (22), Benardina Mwita (18), Maria Mpete (22) na Cythia Baro (22).

Wengine ni Happyness Paul (21), Happy Mushi (20), Neema Chaky (18), Consolata Lukosi (20), Rose Anthony (23), Light Mziray (20), Bellynda Mselewa (20), Harrieth Mulumba (20), Lilian Andrew (19), Selina Wangusu (21) na Doreen Deus (18).

Warembo hao watakutana na majaji kesho kwenye prejudgement. Zawadi za washindi zitatangazwa Alhamisi kwenye kikao cha pamoja na waandishi wa habari itakayofanyika kwenye ukumbi wa Savanna Lounge kwenye jengo la Benjamin Mkapa Towers .

Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” watatumbuiza kwenye shindano hilo ambalo taji lake linashikiliwa na Everlyne Gamasa.

Miss Tabata imedhaminiwa na Vodacom, Overmeer Wine, East Africa Radio, EATV, Chicken Hut, Savanna Lounge, PSI, Fabak Fashion, Dreditto Entertainment, Screen Masters, Benchmark Productions, USA-Dars General Supplies.
Warembo zaidi ya 10 watafuzu kushiriki kwenye mashindano ya kanda ya Ilala na baadaye Vodacom Miss Tanzania.

Shindano la Tabata ni moja ya vituo viwili vilivyobakizwa kwenye kanda ya Ilala baada ya vingine vitatu kufutwa na waandaaji wa taifa.



Miss Tabata namba mbili wa mwaka jana Julieth William ndiye Vodacom Miss Tanzania namba tatu kwa sasa.

Mwisho

Comments