KAMATI MISS TANZANIA KUTEMBELEA KAMBI YA MISS DAR INTER COLLEGE

Toka kushoto Angela Msangi TBC 1 ambaye ni mwandaaji wa Miss Dar Intercollege 2010, Khadija Kalili, Mamapipiro wa Tanzania Daima, Somoe Ng'itu wa Nipashe na Zena Chande wa habari leo tukiwa kazi katika moja ya hafla za Miss Tanzania

KAMATI ya mashindano ya Miss Tanzania leo inatarajiwa kutembelea kambi ya Miss Dar Inter College iliyopo kwenye klabu yenye hadhi ya kimataifa ya Bilicanas jijini Dar es Salaam.


Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mratibu wa shindano hilo, Silas Michael, alisema ziara hiyo ni sehemu ya mchakato wa shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Mei 27 kwenye ukumbi huo.

Silas alisema warembo wanaowania taji hilo watapewa maelekezo ya mambo mbalimbali kuhusiana na mashindano ya urembo, ikiwemo sheria, kanuni na menginyeno kwa ujumla.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Mei 27 ukumbini hapo, ambako warembo watakaoshiriki wanatoka katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu vya Jiji la Dar es Salaam vikiwemo Chuo cha Biashara (CBE), Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na vinginevyo.

Mratibu huyo aliongeza kwamba maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri ambako hadi sasa Kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology Tz Limited, Vodacom Tanzania na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Redd’s Original zimejitokeza kudhamini.

Comments