FILAMU MPYA 'KIZUNGUKUTI YAJA

TUMAINI BIGILIMANA 'FIFII' MTUNZI, MTAYARISHAJI WA FILAMU YA KIZUNGUMKUTI AMBAPO PIA AMEIGIZA

HUSNA POSH 'DOTNATA' MMOJA YA WAIGIZAJI WA KIZUNGUMKUTI

MZEE MAKASSY KINARA WA FILAMU HIYO

ZAMDA SALIM ALIYECHEZA KAMA 'RUTH' KATIKA FILAMU HIYO

MSANII anayekuja kwa kasi katika tasnia ya filamu za kibongo Tumaini Biligilimana ‘Fifii’ ameibuka na filamu yake ya pili akiipa jina la ‘Kizungumkuti’ huku ikiwa mbioni kuingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa.

Katika mahojiano maalum na MNYAWEZI HALISI  yaliyofanyika ofisini kwake Kinondoni mapema wiki hii, Fifii alisema filamu hiyo ni kisa cha kweli kilichowahi kumtokea mmoja wa watu wake wa karibu.

Alisema filamu hiyo ambayo imerekodiwa na kampuni ya Simple Productions ya jijini Dar es Salaam na kuchezwa na wasanii mbalimbali akiwemo yeye mwenyewe, Makasy Kitonzunge ‘Mzee Makasy’, Elizabeth Chijumba ‘Nikita’, Husna Shaban ‘Dotnata’ na Zamda Salim ‘Ruth’.



Akiizungumzia filamu hiyo alisema inamuhusu mama (Fifii) ambaye aliwatelekeza watoto wake baada ya kuachana na mumewe ambapo watoto hao walijikuta wakichangia mapenzi na baba yao mzazi ‘Mzee Makasy’ bila kujijua.
Anasema licha ya kuwa filamu hiyo inahusu mapenzi ina mvuto wa aina yake kwani mtazamaji atakapoanza kuingalia hatotaka kuinuka kwenye kiti mpaka afahamu mwisho wake utakuwaje.

Anaongeza kuwa filamu hiyo ambayo itakuwa na sehemu ya 1 & 2 waigizaji wameubeba uhusika inavyostahili, pia imevikidhi viwango vya sauti na hata mavazi na maeneo yaliyotumika katika upigaji picha.

Fifii ni nani?

Kwa mashabiki wa filamu za kibongo jina hilo si geni masikioni mwao kwani amewahi kushiriki katika filamu lukuki zilizoweza kuteka hisia za mashabiki zikiwemo Cross my Sin, Too Late, Copy, Dar es Salaam, Fake Smile, My Heart na nyinginezo.

Kabla ya kutua jijini Dar es Salaam, Fifii akiwa katika mkoa aliozaliwa Kigoma aliwahi kuitunga, kutayarisha na pia kuwa mmopja ya waigizaji filamu yake ambayo ni ya kwanza aliyoipa jina la ‘Haraka ya Maisha’ aliyoitoa mwaka 2004.

Kama hiyo haitoshi Fifii amekuwa akijishughulisha na mambo mbalimbali ya kijamii sambamba na kuwa mjasiriamali ambapo anaendesha biashara ya saluni ya wanawake pamoja na Boutique.


Mtazamo wake katika soko la Filamu:

Msanii huyo anasema licha ya kuwa soko la filamu za kibongo limeshika kasi kwa kiasi kikubwa unahitajika wigo wa wasambazaji wa kazi hizo.

Anasema kuwepo kwa wasambazaji wengi kutafanya uchaguzi kwa wasanii na hasa wanaochipukia kwani wamekuwa na hofu ya kutokubwaliwa kwa kazi zao.

Aidha, amewataka wasanii kwenda shule kujifunza masuala mbalimbali yahusiananyo na filamu ikiwemo upambaji wa wahusika, uhariri, upigaji picha n.k kwani kwa kufanya hivyo watafanya kazi zao kiujuzi zaidi.
“Pia serikali nayo iitazame tasnia ya filamu katika nyanja mbalimbnali ikiwemo kuwasaidia wasanii kujiendeleza hata kuleta wakufunzi toka nje kwa mafunzo mafupi”, Anasema.

Comments

  1. Kwa jinsi waigizaji walivyonamvuto nahisi itakuwa bomba ile mbaya, msisite kutuhabarisha itakapotoka

    ReplyDelete
  2. Kwanza hongera kwa blog nzuri mamapipiro, pili nampongeza mtunzi wa filamu kwani kwa jinsi ulivyotusimulia nadhani itakuwa bomba sana.
    Keep it up mamaa FIFIIIIIIII

    ReplyDelete
  3. jamani mwaenzenu nampenda sana huyo dada zamda mzur na anajihehim,keep it up

    ReplyDelete
  4. i love u zamda we waukwel dadangu

    ReplyDelete

Post a Comment