AMINI, BARNABA KUTAMBULISHA BILICANAS MEI 27

AMINI KUSHOTO NA BARNABA

WASANII wa bongo fleva Amini na Barnaba toka kundi la THT wanataifanyia utambulisho albamu yao ya pamoja Mei 27 katika klabu ya kimataifa ya Bilicanas kupitia shindano la kumsaka RBP Miss Dar Intercollege.

Wakizungumza ukumbini hapo hivi karibuni wasanii hao walisema albamu hiyo yenye nyimbo 13 wameitayarisha katika studio tofauti zikiwemo Mj, Music Lab, Soundcrafters na iliiingia sokoni wiki iliyopita.
Nyimbo zilizizopo ni pamoja na NJIA PANDA, WRONG NUMBER, MBALAMWEZI, KODIMANGA, MAMA VANESSA, NIMELIMISS, ROBO SAA, WEKEEND, SOO SOO, SIMU YA KAMERA, MBONA UMEKWENDA NA NIVUMILIE.

Comments