13 wachujwa Miss Tabata 2010

WAANDAAJI wa shindano la kumsaka Miss Tabata 2010 kampuni za Bob Entertainment na Keen Arts wamewachuja warembo 13 waliokuwa mbioni kushiriki shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Mei 28 katika ukumbi wa Dar West Park , Tabata.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga, alisema kuwa warembo hao wamechujwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na sifa stahili, mahudhurio hafifu mazoezini na utovu wa nidhamu mbovu.

Kalinga aliwataja warembo waliyochujwa kuwa ni Anna Mwakapala (18), Joyce Joseph Sadick (21), Agatha Killala (20), Maria Joseph (18), Roseline Sekwao (19), Agnes Abdallah (20), Grace Johanes (18), Phina Wilford Urio (19), Esther Herory (19), Mackline Andrew (18), Georgina Zakaria (19), Alice Sidika (23) na Grace Mzamiri (23).

Aidha aliwataja warembo waliobaki kuwa ni pamoja na Ritha Swai (19), Laura Nyaki (21), Upendo Paul (18), Jesca Mariwa (19), Ummy Mohamed (22), Benardina Mwita (18), Maria Mpete (22), Khajida Abdul (19) na Cythia Baro (22).

Wengine ni Happyness Paul (21), Happy Mushi (20), Neema Chaky (18), Consolata Lukosi (20), Rose Anthony (23), Light Mziray (20), Bellynda Mselewa (20), Harrieth Mulumba (20), Lilian Andrew (19), Selina Wangusu (21), Doreen Deus (18) na Ryhinna Jesse (21).

Aliongeza kuwa zoezi la mchujio wa washiriki linaendelea na hasa ikizingatiwa kwamba kambi yao imejaza warembo ambapo waliobaki wanaendelea na mazoezi kwenye ukumbi wa Dar West Park chini ya ukufunzi wa Rehema Uzuia, Stella Solomon na Abdilayi Zungu.

Kalinga alisema kuwa bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” watatumbuiza kwenye shindano hilo ambalo taji lake kwa sasa linashikiliwa na Everlyne Gamasa ambapo Miss Tabata namba mbili wa mwaka 2009 Julieth William alishika nafasi ya tatu katika fainali za Miss Tanzania.

Miss Tabata imedhaminiwa na Vodacom, Overmeer Wine, PSI, Fabak Fashion, Dreditto Entertainment, Screen Masters, Benchmark Productions, USA-Dars General Supplies.

Comments