Kumekucha 'Harusi Trade Fair'

WASHIRIKI 52 wamejitokeza kushiriki maonyesho ya maalum ya masuala ya harusi ‘Harusi Trade Fair’ yanayotarajiwa kufanyika kesho na keshokutwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mwandaaji wa maonyesho hayo ambaye pia ni mbunifu maarufu nchini, Mustafa Hassanali, washiriki hao watashiriki kuonyesha kazi mbalimbali zinazohusiana na masuala ya harusi.
Kadi


hapa  ni uafrika zaidi
                                           
Hassanali alisema lengo la maonyesho hayo ni kutoa fursa kwa watu kuona na kufahamu nani anafanya nini ili iwe rahisi kufanikisha harusi zao pindi watakapohitaji kuzifanya.
Alisema mbali na bidhaa zihusuzo harusi maonyesho hayo yatahusisha pia masuala ya ‘Kitchen Party’, ‘Send Off Party’ na bidhaa zinazoambatana na mambo hayo kama wapishi, wapangaji, wapambaji, saluni, wapigapicha, wabunifu n.k.
Aliongeza kuwa maonyesho hayo ambayo yamedhaminiwa na East Africa Radio na Televisheni, Vayle springs, 2M Media, Global Outdoor, Black fox models, Ultimate security, Daily news, Habari Leo na Oryx gas Tanzania ltd kiingilio kitakuwa sh.2,000.
Aliwataja washiriki hao kuwa ni pamoja na Nadds House Events hire, Ham Bakerie, Zanzibar Hospitality Services, Fanina investment & Catering services,
Dekor Craft,Endepa Event Planners, Luxe Papers,
The Wedding Planners and Fantastic Cards Int, Mercy G Beauty Parlour, paper designsCathy design& décor, petals & Leaves na Oriflame EA LTD
Wengine ni Abriel Mollel, Party Cakes, Vayle Springs LTD, Ak's LTD, Upper Zonal Trading,Nirvana, Mh Gallery, Tanzania Bloggers Network, 8020 Fashions, Rebecca Fashion TZ LTD, my shot catering, Kinara Mobile Studio, Baker's Nest Ltd, Swan Fashion, queens jewellers Ltd, Rimza Ali na TEDDZZZ, Slice Of wedding, MSDesign, Markham Suites, Wain Africa LTD, Touch Spa, The Flying Chefs,Mustafa Hassanali WeddingPia wamo My shot Production,Big Solutions company, Oryx Gas Tanzania LTD, Patners Wedding Shop, khushya, Al-Musawir,Gracella Bride Wardrobe, Malaika Event Design & Rentals, Entertainment & Music Proffessionals, Décor Place,
Modern Catering Equipment Hire, Tally Fashion & Designers na Shear Illusions

Comments