Kili Taifa Cup 2010 Semina, South Beach, Kigamboni

David Minja, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL

Frederick Mwakalebela, Katibu Mkuu wa TFF
Sadi Kawemba Mkurugenzi msaidizi wa kamati ya ufundi TFF

Kifungua kinywa

baadhi ya wanahabari
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro, Aprili 18 iliandaa semina kwa waandishi wa habari za michezo iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun, huko kigamboni, semina ambayo ilikuwa na lengo la kuwapiga msasa kuhusiana na michuano ya kombe la Taifa mwaka 2010.

Mashindano hayo yatakayoshirikisha timu 23 za kimkoa na timu ya Taifa ya Vijana chini miaka 20 'Ngorongoro Heroes' ambao watakuwa waalikwa yataanza kutimua vumbi Mei 8-31 ambapo timu zimegawanywa katika vituo sita ambavyo vitakuwa mkoa wa Dodoma, Iringa, Mtwara, Mwanza,Arusha na Tanga ambapo kila kituo kitakuwa na timu nne.

Akizungumza katika semina hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja alisema kampuni yake ambayo huu ni mwaka wa nne kudhamini mashindano hayo itatumia milioni 850 kufanikisha.

Alisema mashindano lengo la mashindano hayo ni kutoa nafasi ya kuvumbua vipaji vilivyojificha, kunyanyua na kuviendeleza ambapo mikoa 24 itashiriki huku mshindi ataondoka na milioni 35, mshindi wa pili atapata milioni 20, mshindi wa tatu ataopata milioni 10 na mshindi wa nne na watato kila mmoja atapata milioni tano.

Aidha, Minja alisema mfungaji bora, mchezaji bora, kipa bora, mwamuzi bora, kocha bora na timu yenye nidhamu kila mmoja atapata mil.2.

Naye Katibu Mkuu Wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela alisema timu zitakazoshiriki zinatakiwa kusajili wachezaji 20 na vuiongozi watano, pia timu hizo zinaruhusiwa kusajili wachezaji watano wanaocheza ligi kuu bara.

Mwakalebela alisema wachezaji wa Taifa Stars mwaka huu hawataruhusiwa kucheza michuano hiyo, huku wale wa Ngorongoro Heroes watakaoruhusiwa ni wenye umri wa kuanzia miaka 18.

                                                               

Comments