FM ACADEMIA, TWANGA PEPETA

JUZI katika viwanja vya leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kulifanyika mechi ya kirafiki baina ya wanamuziki wa bendi za muziki wa dansi nchini wanaodaiwa kuwa ni mahasimu,African Stars maarufu kama Twanga Pepeta dhidi ya Fm Academia maarufu kama 'Wazee wa Ngwasuma.

Katika mchezo huo ulioteka hisia za mashabiki lukuki wa bendi hizo, wanamuziki hao wakiwa na jezi zenye rangi ya njano (twanga) na nyekundu (Fm Academia) waliudhihirishia umati uliojitokeza kuwa wapo 'fit' pia katika sekta ya michezo na hasa kandanda si jukwaani kwani walionyesha soka la uhakika.

Mpaka mpira unamalizika timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana.

Mnyamwezi Halisi anawatakia kila la heri katika kuonyesha mfano bora kwa jamii ambayo imejenga dhana kuwa wasanii hao hawapikiki chungu kimoja.

Comments