'Field Marshal 'arejeshewa simu zake

SIMU mbili alizopoteza Mwenyekiti wa klabu ya Soka ya Simba, Hassan Dalali 'Field Marshal'katika mkutano wa wanachama uliofanyika jumamosi iliyopita katika hoteli ya Starlight jijini dar es Salaam zimepatikana.

Hatua hiyo inafuatia Dalali kutoa siku saba kwa aliyezikwapua au kuziokota simu hizo kuzirudisha vinginevyo yangemkuta ya kumkuta, mkwara ambao umesaidia kwani kesho yake yaani Jan.17 wakati Simba inacheza na Maji Maji ya Songea katika uwanja wa uhuru, Dalali alirejeshewa simu zake.

Dalali
"Namshukuru Mungu simu zangu zote nimezipata, nawaomba muendeleze ushiruikuiano huu", Alisema Dalali.

Comments