OKWI AKWAMA AUSTRIA


NDOTO za Simba kuvuna kitita cha euro 600,000 kwa klabu ya Red Bull Salzburg ya Austria zimeyeyuka baada ya mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, kushindwa majaribio yake ya kucheza soka ya kulipwa, imefahamika.
Habari za uhakika zilizopatikana jijini Dar es Salaam, zinaeleza kuwa nyota huyo ameshindwa kufuzu majaribio yake yaliyodumu kwa wiki kadhaa.
Awali, viongozi wa Simba walidokeza kuwa nyota huyo amefuzu, lakini amepatwa na malari, hivyo angerejea jijini Dar es Salaam kwa matibabu kabla ya kuendelea na taratibu nyingine juu ya suala lake la kwenda Austria.
“Ni kweli Okwi amefeli majaribio yake Austria, lakini sijui kwanini viongozi wa Simba wameshindwa kuwa wakweli kuhusiana na hili suala,” kilisema chanzo hicho.

Comments