KUELEKEA MECHI YA SIMBA, YANGA PRESHA INAPANDA NA KUSHUKA


SIMBA na Yanga zinakutana katika mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara  kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa nne tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo miamba hiyo kukutana katika michezo tofauti.

Katika mechi nne za awali mwaka huu, Yanga ilishinda moja,huku Simba ikishinda mara mbili na kutoka sare mara moja.

Mapema januari 12 katika fainali za kombe la Mapinduzi Simba ilishinda mabao 2-0.

Yanga inaingia katika mchezo wahuo wiki moja tangu imtimue kocha wake Mkuu Samt Timbe na kumrudisha KostadinPapic, wakati Simba itaendelea kujivunia kocha wake Mganda, Moses Basena.
Simba inaonekana kuwa bora zaidi kwani haijafungwa tangu kuanza kwa ligi hiyo zaidi ya kutoa sare tatu dhidi ya Kagera Sugar, Azam na Toto, wakati Yanga imefungewa mechi mechi mbili na kutoka sare mechi tatu.

Safu ya ushambuliaji za timu hizo zinanaonekana kuwa na makali sawa kwani katika mechi zote 11 za ligi zimevuna mabao 18 ingawa Simba inaonekana kuwa na safu imara ya ulinzi iliyoruhusu mabao manne tu huku Yanga ikifungwa tisa.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali unaotiwa chachu na historia ya timu hizo ambapo kabla ya kukutana zimekuwa zikiingia mafichoni kwa ajili ya kujiandaa.

Wakati Simba itashuka dimbani hapo ikitokea kwenye hoteli ya Blue Pearl Ubungo, jijini Dar es Salaam, Yanga itashuka ikitokea Double Tree By Hilton iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHOctober 28, 2011 at 8:53 PM

    DU!KWA HIYO YANGA ITATOKEA MASAKI SIMBA ITATOKEA UBUNGO BUS TERMINAL!!!TAYARI BAO LA KWANZA HILO!

    ReplyDelete
  2. Simba wangeshinda ungekuwa umeishaweka picha..pole sana dada yangu, ndio soccer hiyo.

    ReplyDelete

Post a Comment