CARTOON ZILIVYOPOTEZA MUDA WA WATOTO KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO



Na Dina Ismail
NAKUMBUKA zamani kulikuwa na michezo mingi sana ya watoto na kila mida ya jioni na siku za mwisho wa juma  watoto walijikusanya katika maeneo ya wazi,  pembezoni mwa nyumba  au katika vibaraza kwa ajili ya kucheza.
Makusanyiko hayo ya watoto yalifanyika baada ya kumaliza majukumu yao ya kishule au kwa wale waliokuwa wakisoma madrassa waliungana na wenzao baada ya kurejea nyumbani.
Kuna michezo iliyohusu watoto wa kike pekee,  watoto wa kiume pekee na kuna michezo ambayo ilihusisha watoto wa jinsia zote.
Michezo kama mpira wa miguu, mdako, kombolela, kujipikilisha, kuruka kamba, kibababa na kimamama, mstari kati, rede, bao, kipande na mingineyo ndiyo ilishika kasi.
Lakini katika miaka ya hivi karibuni utandawazi umeshika kasi  kwa watoto kupendelea zaidi kuangalia ‘cartoon’ pindi warejeapo masshuleni ama ki[pindi cha likizo na mapumziko ya mwisho wa wiki.
‘Cartoon’ zimeteka zaidi  akili za watoto wengi na hasa wa mijini  na hivyo kuwafanya washindwe hata kujihusisha na michezo mingine kama ilivyo kuwa zamani sababu ya cartoon.
Mtoto akikanyaga tu ndani kabla hata hajavua nguo za shule moja kwa moja ataenda washa TV na kuangalia mactaroon kwa dakika kadhaa kabla ya kwenda kubadilisha na kuendelea na burudani yake hiyo.
Kama mzazi usipokuwa mkali mtoto atakaa kakodoa macho kwenye tv mpaka usiku mkali bila hata ya kukumbuka kufanya vitu vingine ikiwemo kazi za shule  au kufanya maandalizi mengine kwa ajili ya shule kesho.
Kwa  jinsi watoto walivyotekwa na Cartoon kuna baadhi huwapa mitihani wazazi wao pindi wanapowafanyia manunuzi ya nguo, mabegi  na vifaa vya shule ambapo hutaka wanunuliwe vilivyo na picha za cartoon wanazozitaka wao;kinyume na hapo hamtaelewana.
Yaani hata wakiwa mashuleni stori zao ni cartoon utasikia sijui cartoon gani mpya imeingia, mara kituo hiki ndio kina carton nzuri, mtoto  anajua hadi ratiba za carton katika vituo vya tv kulikio hata ratiba za masomo shule.
Lakini ukija mwenye michezo,, mtoto hajua hata mchezo mmoja na hata ukijaribu kumuuliza unapenda mchezo hani hana cha kujibu, uliza cartoon sasa utaorodheshwa mpaka uchoke na roho yako.
Sio kwamba cartoon hazifai kwa watoto wetu la hasha ila ziangaliwe kwa muda stahiki kwani zipo cartoon ambazo zina mafunzo mazuri tu kwa watoto, zipo zinazoburudisha.Pia husaidia kuwafunza kujua lugha hasa ya kiingereza kwa ufasaha.
Kwa hali ilivyo, wazazi hawana budi kusiamama kidete kukabiliana na hali hii ili kuhakikisha watoto wanakuwa katika mstari ulioonyooka kwa kufanya vitu kwa kuendana na ratiba.
 Kuna methali isemayo, Samaki mkunje angali mbichi:hivyo ni vema wazazi kusimamia watoto ili kuwarejesha katika kujifunza  michezo na masuala mengine kwa  manufaa ya baadaye.
Kwamba, watoto wasimamiwe kuhakikisha wanakuwa na muda maalum wa kucheza, kufanya kazi za shule na pia kujifunza kazi nyingine ndogo ndogo za nyumbani  bila kuangalia jinsia.
Bila kufanya hivyo tutajikuta tunakosa wanamichezo au ‘watu flan’ wa baadaye kwani bila ya kuanza kujifunza kitu au kuwa na mapenzi nacho tangu utotoni ni vigumu kukifanya ukubwani tena kwa mafanikio.
Wazazi tusaidie walimu katika kusiamamia watoto wetu na tusiwarudishe nyuma walimu kwani kama shule wamefunzwa kitu ni vema  na nyumbani wakaelekezwa kidogo, kutiwa moyo au kuongezewa kiasi ili kumsaidia mtoto.





Comments