STARS IJIPANGE AFCON SIO KUBEZA KUNDI

Na Dina Ismail
WIKI  iliyopita tumeshudia kutolewa kwa  ratiba ya makundi ya  kufuzu fainali za kombe la Mataifa zitakazopigwa nchini Cameroon mwaka 2019, huku Tanzania ikipangwa kundi  L pamoja na Uganda, Cape Verde na Lesotho .
Katika  droo  iliyofanyika mjini Libvreville, Gabon, michuano hiyo itaanzia kwa hatua ya mchujo  kwa mechi kuchezwa  kati ya Machi 20 na 28 huku  mechi za kwanza za makundi zitaanza Juni 5 na 13, za pili Machi 19 na 27 2018, za tatu Septemba 3 na 11, 2018 za nne Oktoba 8 na 16, 2018 na za tano Novemba 5 na 13, 2018.
Katika michuano hiyo,  raundi ya awali itazihusisha timu za Comoros, Djibouti, Madagascar, Mauritius, Sao Tome E Principe na Sudan Kusini.
Kundi L  ukiliangalia kwa haraka haraka linaonekana ni kundi  rahisi zaidi kwa Taifa  Stars, kwani  wapinzani  wake  wote  ni timu ambazo zipo ndani ya uwezo wake.
Kenya pia itaanzia hatua ya makundi, ikiwa imepangwa Kundi F pamoja na Ghana, Ethiopia na Serra Leone, wakati Rwanda ipo Kundi H pamoja na Ivory Coast, Guinea na Afrika ya Kati (CAR).
Mshindi wa kila kundi atafuzu moja kwa moja AFCON ya 2019, wakati timu nyingine tatu zitakazomaliza nafasi ya pili na wastani mzuri zaidi ya nyingine zitafuzu kama washindi wa pili bora.
Timu zitakazofuzu hapo zitaingia moja kwa moja kwenye makundi A, B na C kukamilisha idadi ya timu nne nne. Kundi Ab lina timu za Senegal, Equatorial Guinea na Sudan, B kuna wenyeji Cameroon, Morocco na Malawi na C kuna Mali, Gabon n Burundi.
Makundi mengine ni; D: Algeria, Togo, Benin na Gambia, E: Nigeria, Afrika Kusini, Libya na Shelisheli, G: DRC, Kongo, Zimbabwe na Liberia, I: Burkina Faso, Angola, Botswana na Mauritania, J: Tunisia, Misri, Niger na Swaziland, K: Zambia, Msumbiji, Guinea-Bissau na Namibia.
Cameroon ikiongoza Kundi, mshindi wa pili atafuzu moja kwa moja na kama itashika nafasi ya tatu au ya nne, mshindi wa kwanza atafuzu
Hata hivyo ukiangalia kiundani zaidi Taifa Stars hawapaswi kulidharau kwani mdharau mwiba mguu huota tende hivyo haina budi kujipanga kama inacheza na timu yoyote kubwa.
Kwamba mara nyingi mechi ambazo zinaonekana nyepesi ndio huwa ngumu zaidi kwa vile timu pinzani inakuwa imejiandaa kikamilifu, hivyo kama Stars itaamua kubeteka na kufanya maandalizi ya zimamoto itakula kwetu!
Tayari Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ilishatangaza  Mzalendo, Salum Mayanja kuwa kocha mkuu wa muda  wa Taifa Stars, akirithi  mikoba ya mzalendo mwenzake Charles Boniface  Mkwasa.
Hivyo basi Mayanja atakuwa na kazi ngumu ya kuhakikisha anateua kikosi bora zaidi ambacho kitaweza kufannya vema sio tu kwa Afcon, bali kwa michuano mingine itakayoshiriki akiwa kama kocha mkuu.
Kama hiyo haitoshi umoja na mshikamano baina ya wachezaji, benchi ka ufundi na viongozi wa TFF vyote vinahitajika ili  kuhakikisha timu inakuwa katika ubora wa hali ya juu na hivyo kusaidia kuipatikanan kwa uishindi mnono na hatimaye kutinga fainali.
Katika kuelekea fainali za mwaka huu nchini Gabon, Stars iliiashia hatua ya makundi baada ya kushika  mkia katika Kundi G lililokwa na timu za  Nigeria na Misri.
MAKUNDI KWA UKAMILIFU KUFUZU AFCON 2019
A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Sao Tome/Madagascar
B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoros/Mauritius
C: Mali, Gabon, Burundi, Djibouti/Sudan Kusini
D: Algeria, Togo, Benin, The Gambia
E: Nigeria, Afrika Kusini, Libya, Shelisheli
F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya
G: DRC, Kongo, Zimbabwe, Liberia
H: Ivory Coast, Guinea, Afrika ya Kati, Rwanda
I: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania
J: Tunisia, Misri, Niger, Swaziland
K: Zambia, Msumbiji, Guinea-Bissau, Namibia

L: Cape Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho

Comments