OKWI ANAPOIFANYA SIMBA NJIA YA KWENDEA ULAYA
Na Dina Ismail

EMMANUEL Okwi , nyota wa kimataifa wa Uganda aliyevunja mkataba na klabu ya Sonderjyske ya Denmark, yuko mbioni kurejea katika klabu yake ya zamani ya Simba.Jina la Okwi limekuwa likichomoza mara kwa mara klatika kipindi cha usajili wa wachezaji  Bongo huku akitajwa zaidi katika klabu ya Simba.Hata kipindi cha usajili wa dirisha dogo, uliomalizika  katikati ya Desemba mwaka jana nyota huyo alikuwa akitajwa kurejea Simba, lakini tatizo likawa katika suala la fedha, pia hakuwa mchezaji chaguo wa kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog.Kwamba, kulikuwepo na msigano baina ya viongozi juu ya suala la kumrejesha kundini Okwi ambaye alijiunga na Sonderjyke Julai 2015 akitokea Simba iliyomuuza kwa dola 100,000, ambapo kuna waliotaka arejeshwe na kuna waliokuwa wakipinga.Klabu hiyo ilitaka ilipwe dola 120,000 na Simba ili imuachie Okwi, kitu ambacho kiligomewa na Simba kwa  madai kwamba haiwezekani wamnunue kwa bei ya juu zaidi ya waliyowauzia.Pia kulikwa na taarifa za kuwepo kwa ‘ujanjaunja’ uliotaka kufanywa na kiongozi mmoja wa Simba katika mchajkato huo na ndio maana uongozi uliamua kuacha na mchezaji huyo na kusajili wachezaji wengine wa kigeni.Lakini baada ya Okwi kuvunja mkataba mapema wiki hii kwa madai ya kutopewa nafasi ya kucheza katika klabu hiyo, Simba inaonesha iko tayari kumcrejesha kundini kama mchezaji wake na hasa ikizingatiwa wana udhaifu katika nafasi ya ushambuliaji.Inaelezwa kwamba Okwi atarejea Simba kama mtoto wa nyumbani, yaani hatopewa dau lolote kwa sasa zaidi ya kupokea mshahara tu wa mwisho wa mwezi na posho nyingine ndogondogo.Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za soka za Shirikisho la soka Tanzania (TFF), itakuwa ngumu kwa Simba kumtumia Okwi katika duru la mwisho la ligi Kuu bara kwani zoezi hilo lilishafungwa na ligi sasa hivi inaendelea.Hivyo, Okwi atapaswa kusubiri mpaka msimu usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.Kwa upande mwingine, Okwi anataka kurudi Simba kwa mtazamo wa kuwa mmoja ya wachezaji  wa kikosi cha Taifa ya Uganda, ‘The Cranes’ ambacho kimefuzu kucheza fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Kwamba, kitendo cha kutoitwa katika kikosi cha timu ya Taifa kilimuumiza sana kwani , kocha mkuu wa The Cranes, Mserbia Milutin  Sredojevic  ‘Micho’ alimshauri nyota huyo kujiunga na timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ili iwe rahisi kumfuatilia kwa ukaribu.Kwa upande mwingine, nyota ya Okwi mara nyingi hung’ara zaidi pindi anapokuwa na klabu ya Simba  kwani kwa mara  ya  kwanza  mwaka 2013 simba ilimuuza katika klabu ya E’toile  du sahel ya Tunisia kwa dau la dola 300,.000, kablya  ya kuvunja mkataba na watunisia hao baada ya kushindwa kumlipa mshahara  na kurejea Uganda.Aidha, Okwi alikuja tena Tanzania mwaka 2014 na kujiunga na mahasimu wa Simba, yanga aliyoicheza kwa msimu mmoja tu kabla ya kurejea tena Simba na ndipo ikamuuza  Sonderjyske ya Denmark kwa dau la dola 100,000.