'WASANII HAWA WANA NYOTA YA MAKUNDI'

Na Dina Ismail

MUZIKI wa bongo fleva umekuwa ukishika kasi katika miaka ya hivi karibuni huku tukishuhudia kuibuka kwa wasanii wapya kila kukicha.
Zamani ilikuwa ngumu kwa wasanii mmoja mmoja kufanya vema katika tasnia hiyo, ni makundi tu ndio yalipata wasaa wa kutamba.Ingawa kuna baadhi akiwemo Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ walifanikiwa ckupasua anga wakisimama wenyewe.
Tulishuhudia kufanya vema kwa makundi kama Gansters With Matatizo (GWM), Daz Nundaz, Wateule, Kwanza Unity, Hard Blasters, TIP TOP Connection, Solid Ground Family, East Coast Team, TMK Family  na mengineo ambayo yalisheheni wasanii wenye vipaji vya hali ya juu.
Hata hivyo kuna baadhi ya wasanii waliamua kujiweka kando na kuimba kama wasanii wa kujitegemea, matokeo yake nyota zao hazikuweza kung’ara kama ilivyokuwa ndani ya makundi.
Hawa ni baadhi ya wasanii waliopata umaarufu kupitia makundi, lakini baada ya kuwa wasanii wa kujitegemea wameshindwa kufanya vema licha ya umahiri walionao.

JUMA NATURE:
Nguli huyu wa muziki ni mmoja ya wasanii wenye nyota kali sana.Alitamba zaidi akiwa na makundi ya Wachuja Nafaka,  TMK Wanaume Family, TMK Wanaume Halisi ambapo alikuwa ni msanii mwenye mvuto wa kipekee katika kipindi kile.
Kipindi alipata kutamba na singo kama Ugali, Sitaki Demu, Sonia na nyinginezo na mashabiki walikuwa wakiripuka kwa shangwe pindi alipotajwa kuwa ni zamu yake kutumbuiza katika majukwaa mnbalimbali ya muziki .
Kipindi alipata kutamba na singo kama Ugali, Sitaki Demu, Sonia,  na nyinginezo na mashabiki walikuwa wakiripuka kwa shangwe pindi alipotajwa kuwa ni zamu yake kutumbuiza katika majukwaa mbalimbali ya muziki..
Hata hivyo Nature aliamua kuacha na makundi na kuwa msanii wa kujitegemea na kama ilivyo kwa wengine Nature hakuweza kung’ara sana kama alivyokuwa kwenye kundi.

MCHIZI MOX:
Ni mmoja ya wasanii ninaowapenda na kuvutiwa na kazi zake  kwani kila anapoingiza mashairi lazima kitoke kitu kimoja matata sana.
Mkali huyu anayekwenda kwa jina la Taikun Ally, nyota yake inaonekana kung’ara zaidi anaponya kazi na kundi kwani pindi akiwa kundi na Wateule na wenzake alipata kuwa gumzo kutokana na aina ya uimbaji na sauti yake ya kipekee.
Lakini kundi la Wateule halikuwa kundi mahususi kwani wasanii waliounda ni wale waliounganishwa toka makundi tofauti na ambao tayari walishatoka kimuziki baada ya kufanyika shindano moja la vipaji akiwemo Solo Thang, Jay Moe,Kelvin, Lady Lu, Jaffarie,  Mox na wengineo.
Mox alipata kutamba na nyimbo kama kadhaa zikiwo Vipi Mambo, Kinyumenyume, Piga Makofi na nyingine ambazo alizifanya kama msanii binafsi huku pia akifanya vema kwenye nyimbo za kushirikishwa.
Hata hivyo pamoja na jina la Mox kutokuwa juu kwa sasa lakini bado anaendelea na kazi zake za sanaa.

INSPECTOR HAROUN ‘BABU’:
Mkali huyu wa ‘Rap Cartoon’ alipata kutamba enzi hizo kama mmoja ya waasisi wa makundi ya bongo fleva alipokuwa kwenye kundi la Gangwe Mobb akiwa na swahiba wake Luten Karama.
Gangwe Mob lilikuwa moja ya makundi yaliyokuwa tishio huku vibao kama Tunajirusha, Nje Ndani, rap Katuni na nyinginezo huku Inspector akitoka na nyimbo zake mtoto  binafsi kama Mtoto wa Geti Kali, Asali wa Moyo na nyinginezo.
Baadaye kundi hilo lilichangwanywa na TMK Wanaume family hivyo Inspecta na KArama wakawa wasanii wa TMK na kuendeleza sanaa zao kama kawaida.
 Hata hivyo Inspector alijitoa TMK Wanaume na kisha kuwa msanii wa kujitegemea ambapo hata hivyo alishjindwa kung’ara temna kama ilivyokuwa enzi za ‘Asali wa Moyo’ .

CRAZY GK:
 Katikati ya miaka ya 2000 GK alikuwa mmoja ya wasanii maarufu kupitia kundi la East Coast Team (ECT) lililokuwa na wakali kama Mwana FA, Snare,O -Ten Ay, Pauline Zongo na wengineo.
ECT lilijizolea umaarufu kutokana umahiri walionao wasanii wake kiasi cha kuwa moja ya makundi tishio hapa nchini.
Hata hivyo kundi hilo halikdumu kwa muda mrefu baada ya wasanii wqake kutawanyika kutokana na sababu tofauti.
GK ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wake, tangu kusambaratika kwa kundi hilo ameshindwa kufanya vema kwenye tasnia ya bongo fleva kama ‘solo artist’ licha ya kujaribu kutoa singo kadhaa.

CASSIM  MGANGA:
kwa mashabiki wa nyimbo za mapenzi wengi wanafahamu kipaji chake.
Nyimbo za Awena, Haiwezekani na nyingine ndizo zilizomtambulisha katika tasnia ya bongo fleva huku akifanya kazi chini ya kundi la TIP Top Connection chini ya uongozi wa Batu Tale.
Hata hivyo Cassim alijitoa Tip Top na kufanya kazi mwenyewe.
Hata hivyo ameshindwa kutikisa anga zaidi kama ilivyokuwa zamani licha ya kutoa nyimbo nzuri na zenye ujumbe maridadi.

DAZ BABA:
Wengi mnalilikumbuka kundi la Daz Nundaz ambalo lilipanda kutamba na singo zake kama Barua, Jahazi na nyinginezo.Likiundwa na wakali kama Daz baba, daz Mwalimu,Ferooz na la Rhumba.
Kundi hilo halikudumu sana kwani wasanii wake akiwemo Daz Baba waliamua kufanya kazi binafsi ambapo kwa kiasi kikubwa walijitahidi kutoa vibao vilivyowashika mashabiki.
Daz Baba naye alipata kutoa nyimbo zake kadhaa kama mrembo namba 8, Wife alomshirikisha Ngwair, Nipe tano na nyinginezo, lakini hakuweza kutamba sana kabla ya kupotea kwnye medani ya muziki huo huku akidaiwa kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya.

O- TEN:
Ni mmoja ya wasanii waliopata kutamba miaka ya nyuma akiwa na kundi la ECT.
Jina lake halisi ni Philipo Nyandindi ambapo alipata umaarufu kupitia nyimbo kadhaa zikiwemo Nicheck, Akipendacho binti na nyinginezo.
Hata hivyo tangu kusambaratika kwa East Coast nyota ya O –Ten imeshindwa kuendelea kung’ara.

Z-ANTO:
Ni mmoja ya wasanii waliopata kutikisa katika anga za muziki wa kizazi kipya akitokea kundi la Tip Top Connection.
Z-Anto ambaye mwenye sauti ya aina yake alipata kutamba na nyimbo kama Binti Kiziwi, Mpenzi Jini, Kisiwa cha Malavidavi na nyinginezo.
Hata hivyo Z-Anto alijitoa Tip Top na kisha kutoa nyimbo zake kadhaa ambazo hazikuweza kufanya vema kama alivyokuwa chini ya kundi.

SPARK:
Kwa mashabiki wa nyimbo za kubembeleza, wengi watamkumbuka Spark kutokana kuwa na sauti tamu yenye kuvuta hisia pindi usikilizapo nyimbo zake.
Aliibukia Tip Top connection na nyimbo kama Jela aliomshirikisha Tundaman na Madee, Usinitose aliomshirikisha Chid Benz  na nyinginezo.
Baada ya kujitoa Tip Top nyota yake imefifia licha ya kujaribu kutoa baadhi ya nyimbo lakini ameshindwa kutamba.

Witness Mwijage:
MDADA huyu mkali wa Rap aliibukia katika michuano ya Cocacola Pop Star pamoja na wenzake Sarah Kais ‘Shah’ na marehemu Langa Kileo kupitia kundi la Wakilisha.
Kupitia kundi hilo walipata kutoa kutoa nyimbo kali kama Hoi, Kiswanglish na nyinginezo ambazo zilwaweka katika matawi ya juu.
Hata hivyo kundi hilo halikudumu kwa muda mrefu kabla ya kuvunjika ambapo kila msanii aliamua kufanya kazi kivyake.

Witness maarufu kama ‘Kibonge Mwepesi’ nayo ambaye ni hodari zaidi katika kurap ameweza kutoa nyimbo kadhaa kama msanii wa kujitegemea zikiwemo Zero, Attentio, safari, Buku Jero na nyinginezo  na nyinginezo lakini bado jina lake halikuweza kuwa juu kama alivykuwa na Wakilisha.