ULIMWENGU SIO WA MCHEZO MCHEZO, AKATAA DOLA 400,000 ZA QATARNa Dina Ismail
MSHAMBULIAJI  THOMAS  Ulimwengu amekataa ofa ya dola 400,000 alizopewa na klabu moja ya moja ya daraja la kwanza nchini Qatar.
Ulimwengu  ambaye aliyekuwa akitumikia klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidermokrasia ya Congo (DRC) kwa miaka mitano  kwa sasa yupo nchini baada ya kumaliza mkataba mwezi Oktoba mwaka huu.
Mazembe walitaka kumuongeza Ulimwengu mkataba mwingine lakini alikataa kwa madai anataka kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ualaya.
Mmoja ya waratibu wa mchezaji huyo, aliliambia gazeti hili kwamba, Ulimwengu amekataa ofa hiyo kwani akili yake ipo zaidi katika timu za Ubelgiji.

pamoja na kupokea ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika lakini wameweka malengo mchezaji huyo kusakata kabumbu barani Ulaya.
Aliogeza kuwa, mbali na timu hiyo kutoka Qatar, timu kadhaa zikiwemo Mamelody Sundowns ya Afrika Kusini na nyinginezo zilitaka pia kumsajili lakini amegoma.