KUPUNGUA KWA VITUO VYA SOKA KUMESHUSHA KIWANGO CHA MICHEZO NCHINI


Na Dina Ismail
HAKUNA ubishi kutokuwepo ama kupungua kwa vituo vya kulea vipaji vya michezo nchini ‘Academy’ pamoja na michuano ya mashule kwa ngazi ya msingi (UMITASHUMTA) na sekondari (UMISSETA) kumechangia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha michezo Tanzania.
Hiyo inatokana na maeneo hayo kuwa chanzo cha kupatikana kwa wachezaji chipukizi ambao baadaye wanakuja kuwa tegemeo katika vilabu mbalimbali hapa nchini na timu za Taifa,kiasi ca kushindwa kufanya vema katika michunao ya kimataifa.
Kutofanya vema katika michezo pia  kumepelekea wadau na hata makampuni mabalimbali kupunguza nguvu zao katika kutoa sapoti kwa timu ama timu za Taifa.
Vyama vya michezo mbalimbali nchini vimekuwa vikilia na makampuni ili kusaidia kudhimini timu za michezo husika  badala ya kuimarisha upatikanaji wa wachezaji wazuri ambao uwepo wao kwa timu za Taifa utawavuta kirahisi wadhamini.
Dawa yake ni kuhakikisha vituo vya kzalisha, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana,pamoja na michuano ya mashule inarejeshwa kwa kasi na usimamizi wa hali ya juu.
Kwa kushirikiana na wizara ya habari utamaduni na michezo, vyama hivyo havina budi kuweka mikakati madhubuti katika taasisi hizo ili baadaye tuanze kupata matunda mazuri na kurejesha heshima ya Tanzania.
Licha ya baadhi ya michezo kuonesha kujitutumua katika medani ya kimataifa lakini hali bado si nzuri sana kwani matunda yake yanatokana zaidi na juhudi binafsi za mchezaji kwa kusimamiwa na chama chake kwa ukaribu.
Nchi kama Nigeria, Cameroon, Ghana, Brazil, Misri, Ivory Coast, Marekani, Kenya, Afrika Kusini na nyinginezo ambazo zinafanya vema kwenye michezo mbalimbali zina vituo maalum vya kulea vijana pia vyama vyake vya soka na Serikali  kuwa na ushirikiano wa karibu katika kuviendeleza.Na matunda yake tunayaona.
 Ikumbukwe katika miaka ya nyuma ambapo Tanzania ilikuwa ikifanya vema zaidi katika michezo, wengi wa wachezaji walikuwa wanatokea katika mashindano ya mashule au vituo vya kulea, kukuza na kuendeleza  vipaji.
Baadhi ya wachezaji nyota walikuwa wakitokea katika vituo hivyo hivyo kuwa rahisi kuwepo kwa ushindani na ari kwa vijana wanaojifunza ili kuweza kupata namba katika timu kubwa na hata kuchaguliwa timu za taifa.
Mfano ni mdau mkubwa wa michezo aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo  (BMT) Iddi Kipungu alifanikisha kwa kiasi kikubwa kuzalisha nyota wengi mwishoni mwa miaka ya 1990 ambapo baadhi yao wanatamba hadi sasa.
Kipingu enzi hizo akiwa mkuu wa Sekondari ya Makongo alikuwa akisaka wacezaji wenye vipaji kupitia michauano ya mashule na hata mitaani ambapo aliwachukua wachezaji wenye vipaji toafauti na kuwaingiza shuleni kwake.
Makongo ilikuwa kituo bora kabisa cha uzalishaji wa wachezaji mbambali kwa michezo kama riadha, soka, kikapu, wavi, vishale n.k. Pia  wasanii wa tasnia tofauti ambao kila mmoja alipikwa katika sekta yake na kuiva vizuri sana, kimichezo na fikra pia.
Uwepo wa makongo pia ulileta hamasa kubwa ya kuanzishwa kwa vituo mbalimbali vya michezo ambavyo pia vilijitahidi kwa namna moja ama nyingine kuzalisha nyota mbalimbali.
Hivyo basi, baadhi ya timu zilikuwa zikipigana vikumbo kusasijili wachezaji ambao iliwaona wanafaa kuzichezea timu zao ili ziweze kufanya vema katika michuano inayoshiriki.
Pia faida ya Makongo tuliiona hata kwa timu ya Taifa za Taifa za soka na hata riadha kwani asilimia kubwa ya wachezaji waliokuwemo walitokea hapo.
 Taratibu hali ya ubora  na viwango vya wachezaji imekuwa ikiondoka na matokeo yake Tanzania kujikuta inashuka katika medani ya michezo ya kimataifa.
Ni baada ya Kipingu kustaafu Makongo huku pia vituo vingine vya michezo vikifanya bora liende kabla ya kupotea kabisa.
Hapo katika serikali nayo ilipigaga marufuku kuwepo kwa michuano ya mashule hali hiyo nay ilichangua kushusha kiwang cha michezo kwani mchezaji mzuri huandaliwa tangu akiwa mdogo.Kwa sasa imerudishwa lakini hali bado si nzuri.
Kwa hali hiyo ni wakati wa serikali na wadau wa soka kurwejesha hamasa ya michezo kwa kufufua vituo hivyo, kuanzisha na kusimamia vizuri mashindano ya mashule ili tuweze kufanya vema na kurejesha heshima ya nchi.

Kwa kuonesha umakini kutarejesha hata makampuni ama taasisi ambazo zilikuwa zinatoa fedha kudhamini kabla ya kusitisha kurejea na kutoa sapoti na mwisho wa siku faida tutaiona.

Comments