YANGA WATUA KAGERA, WAJIFUA UWANJA WA NTUNGAMO


elvin Yondani (katikati) akiwa mazoezini jioni ya leo katika viwanja vya shule ya semainari ya Ntungamo mjini Bukoba, kwengine ni Haruna Niyonzima (kushoto) Juma Abdul (kulia)Hamis Kiiza na Dida
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Young Africas leo jioni wamefanya mazoezi katika viwanja vya shule ya seminari ya wakatoriki Ntungamo - Kashura pembeni kidogo ya mji wa Bukoba kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika uwanj wa Kaitaba. Kelvin Yondani aliyeripotiwa na chombo kimoja cha habari kwamba ameondolewa kwenye timu taarifa hizo hazina ukweli kwani mlinzi huyo kisiki wa kati ni miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi jioni ya leo pamoja na kikosi cha Yanga.
Young Africans ambayo iliwasili katika mji wa Bukoba majira ya saa 5 asubhi ikitokea jijini Dar es salaam ambapo ilipitia jijini Mwanza kabla ya kutua kwenye mji huu ambao una mandhari mazuri na hali ya hewa safi.
Kocha mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts ametumia muda wa masaa mawili kuwafua vijana wake 21 ili kuwa fit kuelekea mchezo huo wa jumamosi ambao ni muhimu kwa Yanga kupata pointi 3 ili kujiweka katika mazingira mazuri.
Timu ilipolekelea uwanja wa ndege na umati mkubwa wa wapenzi na washabiki wa Yanga ambao walisema wamefurahia kuiona timu yao tena ikiwa katika mji huu na kusema watashilikiana bega kwa bega kuhakikisha timu inapata pointi 3 kwenye mchezo huo.
Kesho jioni Young Africans itafanya mazoezi katika uwanja wa kaitaba yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo wa siku ya jumamosi.
Wachezaji waliofanya mazoezi leo jioni ni:
Walinda Mlango: Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul
Walinzi : Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', na Kelvin Yondani
Viungo: Haruna Niyonzima, Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo, Nizar Khalfani, Mrisho Ngassa na Saimon Msuva
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson
Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi na Abdallah Mguhi 'Messi'
CHANZO:www.youngafricans.co.tz