PSPF YAWAOMBA WANAMICHEZO NA WASANII KUJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARINilipopokea mwaliko kutoka Mfuko wa Pensheni (PSPF) ukiniomba kuhudhuria kwenye hafla fupi ya chakula cha mchana pamoja na wadau wa tasnia ya sanaa na michezo nchini, sikuelewa mara moja lengo la hafla hiyo lakini baada ya kufika ukumbini na kupata ufafanuzi wa mabadiliko makubwa yaliyofanywa na PSPF nikapata somo.
Kumbe PSPF sasa si kwa watumishi wa umma pekee bali hata wanamuziki, waigizaji, wachezaji na hata watu wengine waliokwenye sekta zisizo rasmi wanaweza kujiunga na kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.
Wadau wengi wa tasnia ya sanaa na michezo walijitokeza kwenye halfa hiyo tukianza na Elizabeth Michael Lulu, Mwanamitindo mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi, Flaviana Matata, Mtitu, Steve Nyerere, Nahodha wa timu ya taifa ya soka wanawake Sophia Mwasikili na wadau wengine wengii...


Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata
Steve Nyerere
Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin

Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin anasema lengo kukukutana na wadau hawa ni kutambulisha kwao mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME-PSS) ambao unamwezesha mtu yeyote kujiunga na mpango huo awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe.

“Uzuri wa mpango huu wa uchangiaji wa hiari, unaruhusu hata wanachama waliokwenye mifuko mingine kujiunga nao lakini pia mwanachama anayohiari ya kuhamia kwenye mpango wa uchangiaji kwa mujibu wa sheria yaani Main Scheme” Anasema Costantina

Anasema kuwa kiasi cha michango kwenye mpango wa hiari kinaanzia shilingi elfu kumi (10,000) kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu ambapo mwanachama yuko huru kuchagua kuwasilisha michango kwa wiki, mwezi au kwa msimu na michango hiyo inawasilishwa kupitia akaunti ya benki, au wakala wa malipo wa M-Pesa na Airtel Money.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu anasema mpango wa hiari ni mkombozi kwa wadau wa sanaa na michezo kwa kuwa utawawezesha kujiwekea akiba itakayowasaidia wakati na hata baada ya kustaafu kufanya shughuli zao.
Katika kuhakikisha kuwa elimu ya uhifadhi inawafikia watu wengi na kuwahamasisha kujiunga na mpango huo waa hiari PSPF imekusudia kuwafanya wasanii na wanamichezo kuwa mabalozi katika kufikisha elimu hiyo kwa jamii.
“Sio jambo rahisi kuielimisha jamii juu ya kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye lakini kupitia wasanii na wanamichezo tunaweza kuleta mabadiliko na kufanya watu wengi kuwekeza katika mifuko ya hifadhi ya jamii” anasema Mayingu
 
Shuhudia picha za tukio zima la hafla ya chakula cha mchana kwa wadau wa sanaa na michezo iliyoandaliwa na PSPF.

Wadau wa sanaa 
 Afisa Mahusioano wa PSPF, Fatma Elhagy akiwa na mtumishi mwenzake
 Afisa Mawasiliano na Masoko wa PSPFHawa Kikeke
 Naibu Mkurugenzi wa Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Juliana Yasoda

Mdau wa sanaa na akiwa na staa wa kesho  
Wadau wa sanaa na michezo 

 Baadhi ya watumishi wa PSPF
 Mshereheshaji katika hafla hiyo, Angela Bondo
 Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa idara mbalimbali wa PSPF
Wadau 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu kwa wanawake, Amina Karuma akiwa na Nahodha wa timu ya Taifa ya soka kwa wanawake Sophia Mwasikili
 Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata

 Mr. Tairo kutoka Bodi ya Filamu Tanzania
 Mdau
Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Jamuhuri Kiwelu Julio nae alikuwepo
 Columba Samjela kutoka Umoja wa Washereheshaji
 Meneja Matekelezo wa PSPF, Amin Labani
Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji PSPF, Frances Mselemu
 Muda wa maakuli
 Mwendo ni 'kujisevia'
  
 Wadau wa sanaa na michezo 
 Baadhi ya watumishi wa PSPF katika picha ya pamoja


Picha