LINK YA KUFATILIA MATOKEO YA NANI MTANI JEMBE


Dar es Salaam: Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imeleta msisimko mpya katika utani wa jadi kati ya mashabiki  wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia kampeni yake mpya ijulikanayo kama NANI MTANI JEMBE iliyozinduliwa leo jijini Dar es salaam na itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Akiongea kwenye uzinduzi, George Kavishe, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lageramesema NANI MTANI JEMBE itawapa fursa ya aina yake mashabiki wa Simba na Yanga kuonyesha mapenzi yao kwa Simba na Yanga kupitia kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa sms ambapo Shilingi milioni 100 zitagawanywa kati ya Simba na Yanga halafu fedha hizo zitawekwa katika benki maalum mtandaoni.
             Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 ambazo zitashindaniwa Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
             Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni 50.
             Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo atapata ujumbe wa kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya  klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi hicho cha sh. 1,000.

             Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na vilevile mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.
             Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na baada ya kutuma sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake na kufanikiwa kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa mashabiki, akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua kulingana upigaji kura.
Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.
Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa kuonyesha mapenzi yao kwa timu zao. Mbali na kampeni ya SMS, kutakuwepo na shilingi milioni 2 ambazo mashabiki watajishindia kila wiki kwa wiki kumi kwa mashabiki watakaoshiriki zaidi. Vilevile Nani Mtani Jembe itawaburudisha mashabiki wa Simba na Yanga kupitia matukio mbalimbali mabonanza, promosheni zitakazofanyika barabarani, kwenye bar na kwenye matawi ya Simba na Yanga. Kampeni hii itafika kileleni tarehe 14 Disemba 2013 ambapo mechi mechi ya hisani itachezwa kati ya klabu hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya maelfu ya mashabiki wa timu hizo. 

Comments