LIEWIG ATUA DAR KUDAI CHAKE SIMBA SC

Na Mahmoud Zubeiry, Kariakoo
KOCHA aliyetupiwa virago mwishoni mwa msimu, Mfaransa Patrick Liewig amewasili leo nchini kwa ajili ya kuja kudai fedha zake, dola za Kimarekani 18,000 za malimbikizo ya mishahara yake akiwa kazini katika klabu hiyo tangu Januari hadi Mei, mwaka huu.
Liewig amelenga mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambayo huwa na mapato mengi na amefikia katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kuwasili nchini, Liewig amesema kwamba amefuata fedha zake na tayari ameanza kumtafuta Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Isamil Aden Rage ili wamalizane.
Nimefuata changu; Kocha Mfaransa wa Simba SC, Patrick Liewig

“Siwezi kuzungumza mengi kwa sasa hadi nitakapokutana na viongozi wa Simba SC, ila nawadai dola 18,000 pamoja na nyongeza ya tiketi ya ndege kwenda na kurudi dola 1, 800,”alisema.
Juni 20, mwaka huu Simba SC ilimlipa Liewig jana dola za Kimarekani 10,000 kati ya dola 26,000 alizokuwa anadai klabu hiyo baada ya kumvunjia Mkataba na kuahidi kumlipa kiasi kilichobaki mwezi huu.
Liewig alikuwa anadai malimbikizo ya mishahara ya miezi miwili, dola 12,000 na akalipwa dola 12,000 za kuvunjiwa Mkataba wakati dola 2,000 ni za tiketi yake ya kurejea kwake.
Kocha huyo alivunjiwa Mkataba wakati amepwa likizo ya kwenda mapumzikoni kwao, baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na nafasi yake amepewa Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’.
Mzee unatafutwa; Liewig anamtafuta Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage

Hata hivyo, baada ya kurejea nchini alifanya mazungumzo na uongozi wa Simba, hatimaye wakakubaliana kulipana kwa awamu, fungu la mwisho likitarajiwa kutolewa mwezi huu.
Liewig alisani Mkataba wa mwaka mmoja na nusu Januari mwaka huu kuifundisha Simba SC akirithi mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick aliyetupiwa virago.     
Katika kipindi chake cha kuwa na klabu hiyo kwa miezi mitano, Liewig aliiongoza Simba katika mechi 25 akiiwezesha kushinda tisa, sare nane na kufungwa saba. 
CHANZO:Bongostaz blog

Comments