USAILI MISS UNIVERSE TANZANIA KUKAMILISHWA KESHO NYUMBANI LOUNGEPRESS RELEASE 
Miss Universe Tanzania chini ya kampuni ya Compass Communications inakamilisha jumamosi 
hii usaili wa warembo jijini Dar es Salaam.
Timu ya Miss Universe Tanzania ilifanya mchakato wa usaili na picha (scouting) katika mikoa 8 
ambayo ni pamoja na Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Manyara, Mtwara na Dar 
es Salaam. 
Miss Universe Tanzania msimu huu utafanya fainali zake mwezi Septemba taehe 27 katika 
ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (NATIONAL MUSEUM), Shaban Robert street jijini Dar es 
Salaam. 
Mashindano ya mwaka huu umepata wafadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mohamed 
Enterprises na Fastjet. Wadhamini wengine watajulikana ndani ya siku chache. Wadhaimini 
wote watatambullishwa wiki ijayo. 

Kuhusu Miss Universe Tanzania:
Miss Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake alikuwa 
Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi yetu ya Tanzania kwa 
kushika nafasi ya Sita kidunia.Mwaka uliofuata, 2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi 
Flaviana Matata na kuvaa taji la Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata 
James mwaka 2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010. Baadae taji lilichukuliwa na Nelly 
Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo Winfrida Dominic. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na MWANAKOMBO SALIM 0655 441165, SEIF KABELELE-
0713302075 USAHILI WA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA KESHO TAREHE 7-9-2013 PALE NYUMBANI LOUNGE KUANZIA SA NNE ASUBUHI.