TAMASHA LA KUSAKA VIPAJI VYA SANAA KUFANYIK MWEZI OKTOBA

Ndugu  Waandishi  wa Habari.
African Star Entertainment – ASET  ikishirikiana na  studio ya  Fleva   Inc  Audio Records  and Video Production   Pamoja na Makubi Sports Promotion imeandaa Tamasha la vipaji vya Wasanii wa fani  mbalimbali  za sanaa kwa Wasanii ambao bado hawajapata fursa ya kutoka na kufanikiwa kupitia sanaa zao, tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi  Octoba ambalo litaitwa  Tamasha  la  Vipaji  2013.

Ndugu Waandishi , Malengo mahsusi ya Tamasha  la Vipaji  2013   ni kuvionesha vipaji mbalimbali vya Wasanii ambao bado hawajapata fursa ya kuonekana  pia kuhamasisha, kuendeleza na kulinda  vipaji vya wasanii  hao ili vipawa hivyo viwe ni sehemu ya nyenzo muhimu ya ajira za uhakika  katika maisha ya vijana mbalimbali ambao wamejiingiza katika taaluma ya sanaa. Tamasha hili pia litasaidia ukuzaji wa ajira za Wasanii mbalimbali  wataojitokeza.

Ndugu Waandishi, walengwa wakuu wa Tamasha  la Vipaji  2013 ni
Wasanii wa Maigizo ya jukwaani (Matangazo , Filamu & Tamthilia),Wasanii wa Vichekesho,Wasanii wa Muziki Bongofleva (R & B, Raga, Hiphop n.k),Wasanii wa Kupiga na kucheza Ngoma za Asili,Wasanii wa kucheza muziki wa Wasanii wa ndani au nje ya nchi,Kucheza show za nyimbo mbalimbali za ndani na nje
Kuigiza Sauti za watu mbalimbali walio maarufu wa hapa Tanzania,Kuigiza kazi za Watangazaji maarufu wa vipindi vya Radio na Televisheni vya Tanzania.
Wasanii wa Ubunifu wa michoroWasanii wenye vipaji vya utangazaji wa vipindi vya radio na televisheni,pamoja na wale wa Sanaa za maonesho ya mavazi

Ndugu Waandishi, Wasanii wataofanya vizuri katika tamasha hilo wapata fursa ya kufanya kazi (lebo) na Studio ya Fleva Inc Record, pia kushiriki katika kazi zinazoandaliwa na ASET ikiwemo filamu, tamthilia kuimba ,kucheza dance n.k. Pamoja na pia tunakaribisha kampuni /taasisi mbalimbali kusaidia kufanikisha tamasha hili pamoja na kuwasaidia Wasanii hawa  kufikia malengo

Ndugu Waandishi, Fursa hii ni adimu kwa Wasanii wengi hivyo Wasanii wanaohitaji  kushiriki wafike Ofisi za ASET au Fleva Inc Studio zilizopo Ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni  kwa ajili ya Kujiandikisha, mwisho wa kujiandikisha ni  tarehe 30 Septemba 2013 saa kumi jioni,tamasha linatarajiwa kufanyika 21 Octoba 2013 katika Ukumbi wa Vijana Hall uliopo Kinondoni mjini Dar es Salaam.

Nawashukuru  kwa  usikivu wenu tunaomba ushirikiano.

W.R  MAKUBI
Project Meneja

Kwa  Niaba
ASHA  BARAKA
Mkurugenzi
                                                  ASET/FLEVA  INC RECORDS