MSANII WA TAARAB PRINCE AHMED MGENI AFARIKI DUNIA

MSANII wa muziki wa Taarab Prince Ahmed Mgeni amefariki dunia alfajiri ya leo Visiwani Zanzibar.
Mgeni alikutwa na umauti huo baada ya kuugua TB ya tumbo kwa muda mrefu anatarajiwa kuzikwa leo visiwani humo.
Enzi za uhai wake msanii huyo aliyepata kuimba katika bendi mbalimbali sambamba na kutoa nyimbo kadhaa zilizoteka alikutwa na umauti huo alipokuwa amelazwa katika hospitali ya mnazi mmoja, Zanzibar.
Moja ya kibao kilichompataia umarufu kilijulikana kama Sitetereki "Mlinzi wa kweli ni Mungu aso hiyana na mtu sio wewe mlimwengu hunibabaishi kitu, anipacho kinatosha pumzi ndo kila kitu, hautonibabaisha kwa kuwa nawe ni mtu, kama ukinithamini nami nitakuthamini ukiona kwa kazi gani nami potelea mbali!.  R.I.P Prince Ahmed Mgeni.