KIGGI MAKASSI KUAGA KESHO, SIMBA IKIIVAA MAFUNZO

TIMU za Simba ya Tanzania Bara na Mafunzo ya Zanzibar zipo jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wao wa kujipima ubavu utakaopigwa kesho katika Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Siumba inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo imesimama kwa muda itautumia mchezo kukipima uwezio kikosi chake, huku Mafunzo ambayo inashiriki Ligi Kuuu Visiwani Zanzibar itautumia mchezo huo kujiandaa na ligi hiyo inayoanza mwezi huu.
Aidha, Simba itautumia mchezo huo kuwatambulisha wacvhezaji wake wapya kwa mara ya kwanza kwa mashabiki wa jiji la Dar es Salaam wakiwemo Gilbert Kaze na Amisi Tambwe kutokka Vital O ya Burundi  sambamba na kiungo wake wa zamani Henry Joseph Shindika aliyekuwa akicheza soka la kulipwa katika klabu ya Kongsvinger ya nchini Norway.
Kama  hiyo haitoshi,  mechi hiyo itatumika na klabu kwa ajili ya mchezaji wake, Kiggi Makassi, ambaye atawaaga washabiki rasmi kwa ajili ya safari yake ya kwenda nchini India anakokwenda kwa matibabu ya goti lake. Kiggi anatarajiwa kuondoka jijini Septemba tisa mwaka huu.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga, mara baada ya klabu hiyo kukamilisha michezo yake miwili katika mikoa ya Tabora na Arusha kwenye mechi mbili za awali za Ligi Kuu ya Tanzania, timu ya Simba imerejea salama jijini Dar es Salaam ikiwa na kikosi chake kamili tayari kujiandaa na mechi ijayo ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro iliyopangwa kuchezwa Septemba 14 mwaka huu.
"Kama sehemu ya maandalizi ya mechi hiyo, kikosi cha Simba kitashuka dimbani katika Uwanja Mkuu wa Taifa siku ya kesho, Jumatatu Septemba 2, kucheza na Mafunzo ya Zanzibar katika mechi ambayo ina faida nyingine zaidi ya kuwa ya kujiandaa na mechi ya Mtibwa", alisema.
Kwa vile Septemba 2 inaangukia siku ya kazi, waandaaji wa pambano hilo wamepanga ianze saa 11 jioni ili kutoa nafasi kwa wapenzi wengi zaidi kuhudhuria pambano 

Comments