HATUJABWETEKA NA USHINDI - JULIO

WEKUNDU  wa msimbazi, Simba Sc wamesema ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mtibwa Sugar jumamosi hautawafanya wabweteke, badala yake umewapa chachu ya kuendelea kujinoa zaidi.
Kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema leo kwamba kikosi chake kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mechi zake za ligi kuu bara ukiwemo wa keshokutwa dhidi ya Mgambo Shooting.
"Ushindi wa juzi hauwezio kutufanya tubweteke, ligi ni ngu,mu hivyo tunaendelea kujipanga kila siku ili tuweze kuhimili mikimiki na hatimaye kushinda,"alisema
Julio aliongeza kwamba kikosi chake kilichopiga kambi katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kipo katika hali nzuri.