HADIJA MSWAGA KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE FAINALI ZA DUNIA ZA MISS UTALII ZITAKAZOFANYIKA NCHINI EQUATORIAL GUINEA

Mshindi wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hadija Saidi Juma Mswaga, ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2012/13, ataondoka nchini 28-9-2013 kwenda nchini Equatorial Guinea, ambako Fainali za Dunia za Miss Tourism World 2013/14 zinafanyika Tarehe 12-10-2013 katika ukumbi wa kimataifa wa Sipopo Conference Centre Malabo Equatorial Guinea. 
Kwa mujibu wa Taarifa iliyo tolewa na Fredy Njeje, mkurugenzi wa Habari na Masoko wa Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), jumla ya washiriki kutoka nchi 126 Duniani watashiriki katika mashindano hayo ya Dunia,ambayo mwaka Jana yalifanyika nchini Thailand ambapo mrembo Tatyana Maksimova kutoka nchini Urusi alishinda  Taji la Miss Tourism World 2012/13.
Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Tanzania kushiriki mashindano hayo ya Miss Utalii Dunia, ambapo kila mwaka kuanzia mwaka 2005 tumeshinda mataji, Mataji hayo na washindi kutoka Tanzania katika mabano ni Miss Tuourism World 2005- Africa (Witness Manwingi – Tanzania), Miss Tourism World 2006 – SADC (Killy Janga – Tanzania), Miss Tourism World 2007 – Africa (Lillian Cyprian – Tanzania), Miss Tourism World 2008- Internet ( Lilly Kavishe – Tanzania) na Miss Tourism Model Of The World 2006 –Personality ( Witness Manwingi – Tanzania).  
Tangu mwaka 2008, Tanzania haikushiriki katika mashindano hayo kutokana na kutokana na kukosa wadhamini wa safari hizo na matatizo mengine ya kiufundi yaliyo pelekea mashindano hayo kutofanyika nchini tangu 2008- 2010.
 Njeje alisema kuwa, Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hajija Saidi Juma Msugwa, anajukumu zito zaidi ya washiriki wengine wote walio tangulia kwani anakazi ya kwenda kulinda heshima ya Tanzania na kudumisha rekodi ya Miss Utalii Tanzania ya kutokushindwa katika mashindano yoyote ya kimataifa na Dunia.
Nae Miss Utalii Tanzania 2012/13, Hajija Saidi Juma Mswaga, amesema kuwa anatambua jukumu kubwa na zito alilonalo la sio kutangaza Utalii na Utamaduni wa Tanzania tu, bali kulinda heshima ya Tanzania na Mashindano ya Miss Utalii Tanzania ya kutowahi kushindwa katika mashindano yoyote ya kimataifa. 
“Nawaomba watanzania waniombee na kunipa ushirikiano wa hali na mali katika kufanikisha maandalizi yangu na safari ya kupeperusha bendera ya Taifa katika medani ya kimataifa”. Shindano la Miss Tourism World 2013, litarushwa na kuonyeshwa LIVE katika nchi zaidi 130 Duniani kote na kushudiwa na zaidi ya watazamaji 650 Milioni Duniani kote, huku washiriki wakipewa fulsa ya kuonyesha vivutio vya utalii vya nchi zao, kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya Televisheni, Majarida na Mitandao.

Comments