FAINALI VODACOM DANCE 100% ZAFANA

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, akikabidhi kikombe cha ushindi kwa kundi la The Choclate, baada wa kuibuka washindi katika fainali za mashindano ya kucheza ya Vodacom Dance 100%, zilizofanyika katika viwanja vya Don Bosko Oster bay. Kundi hilo lilinyakua kikombe pamoja na fedha taslim Shilingi milioni 5

Dar es Salaam, Septemba 1,  2013 ……..  Hatimaye mbabe wa mashindano ya  kucheza nchini amefahamika mwisho wa wiki hii baada ya kundi la The Choclate la Dar es Salaam kuibuka kidedea na kunyakua fedha taslim shilingi milioni tano pamoja na kikombe.
Fainali hizo zilizofanyika katika viwanja vya Don Bosko upanga zilihudhuliwa na mamia ya mashabiki walioshuhuia makundi matano yakitoana jasho vilivyo katika raundi ya kwanza ambayo kila kundi lilikonga nyoyo za mashabiki.
Patashika ilikuwa pale ambapo kila kundi lilichagua karatasi yenye wimbo ambao watatakiwa kucheza bila kujua ni nyimbo gani, katika raundi hii kundi la Wakali Sisi lilikonga nyoyo za mashabiki kwa kucheza vilivyo huku wakiwa wamevalia nguo za kike.
Kundi la the chocolate lilifanikiwa kwa kukonga nyoyo na mashabiki kwa staili yao ya kutambaa kwa tumbo ambapo uwanja mzima ulilipuka pale mchezaji mmoja wa kundi hilo alipoanza kutembelea tumbo kwa umabli mrefu.
Ilikuwa kazi ngumu kwa majaji wakiongozwa na gwiji la kucheza nchini Super Nyamwela, na mtaalam wa kutengeneza video Adam Juma, ambapo iliwabidi kuyarudisha tena makundi mawili uwanjani kurudia kucheza baada ya kufungana kwa pointi ambapo kundi la wakali sisi liliibuka kidedea.
Baada ya kutangazwa kwa mshindi wa tatu na nafasi hiyo kuangukia kwa kundi la Wakali Sisi kazi ilibaki kwa kundi la the Choclate na DDI Crew ambapo mashabiki walikuwa wakipiga kelele huku wakitaja makundi yote, hatimaye mshindi alitangazwa na nafasi kwenda kwa The Choclate na kuibuka na kikombe pamoja na fedha taslim shilingi milioni tano huku kundi la DDI crew likiambulia shilingi milioni moja na nusu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi Mkuu wa kitengo cha Masoko na mawasiliano Kelvin Twissa alisema wao kama Vodacom wanaona fahari kuwa sehemu ya kuendeleza ajira kwa vijana kupitia burudani.
“Tunafuraha sana siku ya leo kama unavyoona mamia ya watu wamejitokeza kuja kuwaangalia vijana wenzao wakitoa burudani badala ya kuwa wamekaa vijiweni, kama Vodacom tunaahidi kuendelea kuunga mkono shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana katika sekta mbalimabli za kielimu na nyinginezo.” alisema Twissa.