CHEKI JAHAZI MODERN TAARAB ILIVYOPAGAWISHA MASHABIKI KATIKA UKUMBI WA DAR LIVE

Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki walifurika Dar Live.
Mashabiki wakiwa wamembeba juujuu mlemavu ambaye alipagawa na burudani za Jahazi.
Khadija Yusuf akijinafasi stejini.
Jukwaa likiwa juu wakati Leila Rashid akiwapa raha mashabiki.
Mzee Yusuf (kushoto) akiwa na Dude 'Yahaya' wakiimba kwa pamoja.
Mzee Yusuf akiendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live.
Mcharaza gitaa wa Jahazi, Musa Musa akiwa kazini. Pembeni ni mabango ya wadhamini.
Wanamuziki wa Jahazi wakiimba kwa pamoja.
Leila Rashid akiwapagawisha mashabiki.
Baadhi ya wasanii wa filamu wakiwa jukwaani kusalimia mashabiki.
Baadhi ya mashabiki waliofurika wakiserebuka.
Mzee Yusuf akiserebuka na mpiga gitaa wa bendi hiyo, Mauji.
Hata sehemu ya kutema mate haikuwepo kwa jinsi mashabiki walivyofurika.
BENDI ya Jahazi Modern Taarab usiku wa kuamkia leo imefunika vilivyo katika onyesho lao la nguvu lililofanyika ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.
Shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf na kundi lake ilizikonga nyoyo za mashabiki na kuwaacha roho safi.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)