BANDARI YA KENYA KUIVAA COASTAL UNION J'2

TIMU ya soka ya Bandari ya Kenya inatarajiwa kuja nchini kwa ajili ya kukipiga na Coastal union ya Tanga, mchezo utakaofanyika Jumapili kwenye uwanja wa Mkwawani jijini Tanga.
Mratibu wa mchezo huo, George Wakuganda amesema leo kwamba mchezo huo wa kirafiki una lengo la kuzipima timu hizo zinazoshiriki ligi Kuu.
Alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanakwenda vema ambapo Bandari inatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa.