YANGA KUJIPIMA NA MTIBWA SUGAR J'2

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga Sc wanatarajiwa kujipima nguvu na Mtibwa Sugar ya Morogoro, mchezo utakaopigwa jumapili kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako amesema kwamba mchezo huo ni mahususi kwa ajili ya kuvima vikosi hivyo vinavyojiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.
Alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika na kwamba amewaomba masdhabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kushihudia viwango vya wachezaji wao.