TUNDAMAM, JUMA NATURE KUPAMBA TAMASHA LA SIMBA DAY,KIINGILIO BUKU 5

WEKUNDU wa Msimbazi Simba Sc wamejinasibu ya kushinda mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya SC Villa ya Uganda jumamosi, mchezo ambao ni mahususi kwa kuadhimisha miaka 77 ‘Simba Day’ tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo, utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala alisema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kuweka historia ya kushinda kwa mara ya kwanza katika maadhimisho hayo.
“ Kama ilivyozoeleka timu yetu kufungwa katika mechi zake za  maadhimisho ya Simba Day , sasa mwaka huu tunataka tuvunje mwiko huo”, alisema 
Alisema wachezaji wa timu hiyo wapo katika hali nzuri wakiendelea na kambi yake katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. 
Aliongeza kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanakwenda vema ambapo kabla ya mchezo wa Villa na Simba kutatanguliwa na mchezo kati ya timu ya vijana ya Simba na timu ya Vijana ya Twalipo. 
“Pia siku hiyo tutatambulisha jezi zetu mpya pamoja na baadhi ya wachezaji wetu wapya tulioweasajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu bara na michuano mingine,”alisema 
Mtawala aliongeza kuwa katika kunogesha tamasha hilo , kurakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature na Tundaman. 
Aidha kiingilio cha chini katika tamasha hilo ni sh 5,000 kwa weatakaokaa viti vya kijani, sh 8,000 kwa viti vya viti vya rangi ya Chunga, sh. 10,000 kwa VIP C, sh.15,000 kwa VIP B na sh 20,000 kwa VIP A.