TIMU YA TAIFA YA NGUMI KUKABIDHIWA MSAADA KESHO

Mkurugenzi wa St. Merry School  na New Palm Hotel iliyopo Bagamoyo, Ndugu Mutta Rwakatale kesho ijumaa, saa 6.30 Mchana katika ofisi za Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) zilizopo karibu na uwanja wa ndani wa Taifa (indoor stadium)  atatoa vifaa vya mazoezi na nauli kwa wachezaji wa timu ya taifa inayofanya mazoezi uwanja wa taifa wa ndani kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa, tukianzia kushiriki  mashindano ya ubingwa wa Afrika yatakayofanyika kuanzia Sept. 01-07/2013 nchini Mauritius, Mashindano ya Jumuiya ya Madola 2014, Mashindano ya Afrika 2015 Mashindano ya Olimpiki 2016 na mengine mengi.
BFT tumefurahishwa mno na mwitikio wa Mkurugenzi huyo kwa kusikia na kuguswa kuhusu timu ya taifa ya ngumi na BFT tunaona   msaada huo umekuja kwa muda mwafaka kwa kuwa timu yetu ya taifa  inafanya mazoezi katika hali duni, kwa kutumia vifaa ambavyo  vimechakaa, lakini pia wachezaji walikuwa wanafika mazoezini kwa kujitolea wao kama wao kwa nauli zao, hivyo tunaamini msaada huo utaleta hamasa zaidi kwa wachezaji kipindi hiki kilichobakia kabla ya kwenda kushiriki mashindano ya ubingwa wa Afrika nchini Mauritius, kwani tunaamini sasa ratiba ya makocha itafanyika kama walivyopanga na wachezaji wataweza kufika wote mazoezini na kwa wakati. 
BFT tunawaomba watanzania wengine wajitokeze zaidi kusaidia timu yetu ya taifa ili uwakilishi katika mashindano ya kimatifa uwe wenye tija.kwa kuzingatia kuwa watanzania wote ndio wanachohitaji na ili kitimie mabondia lazima tuwaandae vema. 
Pia naomba sana vyombo mbalimbali vya habari kujitokeza katika hafla hiyo fupi kwa nia ya kuhamasisha ili watanzania wengine kujitokeza kuendelea kusaida zaidi maana bado msaada unahitajika wa vifaa vya mazoezi, matibabu, chakula, maji,nauli, nguo za mazoezi na posho


Comments