RAY C, THT KUPAMBA MISS ILALA KESHO, MSHINDI KUONDOKA NA MIL 1.5

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Miss Ilala William malechela 'Le Mutuzi' (mwenye Mic)akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kuhusiana na shindano hilo.

WAKATI shindano la kumsaka Redd’s Miss Ilala 2013 likitarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam, mrembo atakayetwaa taji hilo atazawadiwa fedha taslimu sh mil.1.5.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shindano hilo, William Malechela amesema kwamba, jumla ya warembo 14 watachuana kuwania taji hilo.
Alisema mshindi wa pili ataondoka n ash. Mil.1, mshindi wa tatu atapata sh.700,000, mshindi wa nne ataondoka n ash 400,000 na wa tano atazawadiwa sh.300,000, huku washiriki waliosalia kila mmoja ataondoka na sh 200,000.
“Pia mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapata ofa ya kufanya mazoezi ya viungo katika kituo cha Rio Gym & Spa kilichopo jengo la Quality Centre ambapo gharama zake ni sh mil.900 kwa kila mmoja,”alisema
Aliongeza kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yamekamilika huku akisisitiza wadau wa tasnia hiyo kujitokeza kwa wingi katika ukumbi huo ambapo viingilio ni sh 50,000 kwa viti maalum n ash. 30,000 kwa viti vya kawaida.
Aliwataja warembo watakaopanda jukwaani leo kuwania taji ni pamoja na Alice Isaac, Clara Poul,Anna Johnson,Irene Mwelolo, Munira Mabrouk,Rehema Mpanda, Shamim Mohamed, Martha Gewe, Diana Joackim, Natasha Mohamed, Dorice Mollel, Pendo Lema, Kazumbe Mussa na Kabula Kibogoti.
na Noela Michael (2012).
Aidha, shindano hilo ambalo litapambwa na burudani kutoka kundi la Tanzania House Of Talent (THT), Wanne Star na mwanadada Rehema Chalamila ‘Ray C’ limedhaminiwa na Redd’s, Dodoma Wine,CXC Tours,Chilly Will,Tanzania Daima,Jambo Leo,Clouds FM,,City Sports Lounge Times FM, Kitwe General Traders, Rio Gym & Spa, Fredfito Entertainment, Smile Internet na  Blogu ya Wananchi.