OLOYA AIKANA YANGA, ASEMA MIPANGO YAKE NI KUICHEZEA SIMBA IWAPO...


KIUNGO Mganda Moses Oloya ambaye yupo katika mazungumzo na klabu ya Simba ameshangazwa na taarifa kwamba amejiunga na mahasimu wao wa jadi nchini, Yanga.
Oloya amemwambia  mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage kwa njia ya simu kutoka nchini Uganda, Oloya amewataka mashabiki wa Simba kuzipuuza taarifa hizo kwani yupo katika mazungumzo na uongozi wa Simba na mambo yakienda vizuri atamwaga wino kwa ajili ya kuichezea.
"Ninashangazwa na taarifa za mimi kujiunga Yanga, mimi ninafanya mazungumzo na viongozi wa Simba na kama mambo yakienda vizuri nitakuja kuichezea Simba ambayo ipo akilini mwangu,"alisema Oloya