LIGI KUU ENGLAND YAUSOGEZA SIKU MOJA MBELE MCHEZO KATI YA SIMBA V MAFUNZOMICHEZO ya ligi kuu England baina ya Manchester United dhidi ya Liverpool na ule baina ya Arsenal na Tottenham Hotspurs itakayopigwa jumapili imepelekea kusogezwa mbele kwa siku moja  mchezo wa kujipima nguvu baina ya Simba na Mafunzo ya Zanzibar.
 Mchezo wa Simba na Mafunzo uliokuwa ufanyike keshokutwa (jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, sasa utafanyika jumatatu katika dimba hilo kuanzia saa tisa alasiri.
Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala ameiambia SPORTS LADY BLOG  kwamba wameamua kuuslogeza mbele mchezo huo kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa soka ambao wametaka uahirishwe ili kupata fursa ya kuishuhudia michezo hiyo.
“Kama manavyojua mashabiki wa soka ndio wale wale hivyo kutokana na jumapili kuwepo na mechi hizo mbili muhimu hivyo tumeona hatuna budi kusikiliza maombi yao na kuusogeza mchezo huo,”alisema Mtawala
Aidha, mechi baina ya Simba na Mafunzo pia itatumika kuwatambulisha nyota wa,ke wapya  watatu Gilbert Kaze, Amisi Tambwe kutoka nchini Burundi  na aliyekuwa nahodha wa zamani wa timu hiyo, Henry Joseph Shindika.
Kaze na Tambwe ambao itakuwa ni mara yao ya kwanza  kuonekana kwa mashabiki wa jiji la Dar es Salaam baada  ya kukokekana katika  tamasha la Simba Day lililofanyika Agosti 10 mwak huu kwenye Uwanja wa Taifa.
Huku kwa upande wa Henry, ambaye alikuwa akikipiga katika klabu ya Kongsvinger ya Norway aliyojiunga nayo mwaka 2009 akitokea Simba, amerejea tena nyumbani baada ya mkataba wake kumalizika mwezi uliopita.