KIIZA AKUBALI YAISHE YANGA BAADA YA KUONGEZEWA DAU

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga Hamis Kiiza amekubali kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu hiyo baada ya suala lake la kuongezwa maslahi kutimizwa.
Awali, Kiiza raia wa Uganda aliyejiunga na Yanga mwaka 2011 akitokea URA ya huko, alikuwa katika mvutano wa kimaslahi na uongozi baada ya kugoma kuongeza mkataba mpya mpka atakapopandishiwa dau.
Hata hivyo, Yanga walionekana kutotilia maanani sana msimamo wa Kiiza na hivyo kuanza jitihada za kusaka mbadala wake na ndipo waliangukia kwa mchezaji kutoka Nigeria ambaye hata hiovyo alishindwa majaribio yake baada ya kuandamwa na majeruhi.
Baada ya kukwama kumsajili Mnigeria huku tarehe za kufungwa dirisha la usajili zikiwa zinakaribia ndipo Yanga waliporudisha nguvu zao kwa Kiiiza na hatimaye juzi alitua nchini na kusaini mkataba wa miaka mitatu.