HENRY JOSEPH KUKARIBISHWA NYUMBANI J'2

NAHODHA wa zamani wa Simba Henry Joseph Shindika ataungana na nyota wa kimataifa wa timu hiyo Warundi Gilbert Kaze na Amisi Tambwe katika mechi maalum ya kuwatambulisha itakayozikutanisha Simba na Mafunzo ya Zanzibar katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakati Henry amerejea kwa mara nyingine Simba baada ya kumaliza mkataba wa kuichezea Kongsvinger ya Norway mwezi uliopita, Kaze na Tambwe ambao itakuwa ni mara yao ya kwanza kuonekana kwa mashabiki wa jijini Dar es Salaam kwani hawakuwepo katika tamasha la maadhimisho ya klabu hiyo 'Simba Day' ambalo liliambatana na utambulisho wa wachezaji na jezi mpya.
Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala, ameiambia SPORTS LADY BLOG hii leo kwamba maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vema na kwamba kikosi cha Simba kilichokuwa Arusha kwa mchezo wakew wa Ligi kuu bara dhidi ya JKT Oljoro kinatarajiwa kurejea jijini kesho.
"Nawaomba mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi siku hiyo kuwashuhudia wacvhezaji wetu wapya,"alisema
Ikumbukwe kuwa Henry alijiunga na Kongsvinger mwaka 2w009 akitokea klabu ya Simba.