GET TOGETHER FOOTBALL FESTIVAL 2013 KUENDELEA JUMAPILI VIWANJA VYA TABATA SHULE

BONANZA maalum linalohusisha mpira wa miguu 'Get Together Football Festival 2013' litaendelea tena jumapili ya Agosti 25 katika viwanja vya Tabata Shule.
Mratibu wa bonanza hilo, Rodger Peter amesema kwamba bonanza hilo linalohusisha timu 20 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, siku hiyo itafanyika fainali ambapo timu nane ziklizotinga hatua hiyo zitakwaana.
Amesema maandalizi yanakwenda vema ambapo lengo la tamashga hilo ni kudumisha michezo kama afya kwa jamiii hususani maveterani ambao umri wao umesonga mbele.
Rodger aliongeza kuwa michezo ya fainali itakuwa kati ya TABATA KIMANGA v TABATA VETERANI (SIGARA), TABATA SHULE v TABORA VETERAN, TABATA RANGERS v SHEKILANGO VETERAN na NDUMBWI VETERAN v TABATA DAMPO.
Aidha,mshindi ataibuka na seti moja ya jezi, huku mshindi wa pili atapata mipira mitatu na watatu atazawadiwa mipira miwili.