BEKI MWINGINE WA KIMTAIFA ATUA SIMBA, KUTAMBULISHWA JUMAMOSI U' TAIFA


BEKI  wa kimataifa wa Simba Gilbert Kaze aliyekuwa anakipiga Vital’ O ya  Burundi anatarajiwa kuwasili jioni ya leo na kama mambo yatakwenda vema  atasaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba katika michuano mbalimbali itakayoshiriki pamoja na Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
 “Tunashukuru kwamba nafasi ya beki wa Kati ambayo ilikuwa na mapungufu imepata wahusika hivyo, Kaze sasa ataungana na Mganda Joseph Owino ambaye pia ni mchezaji mpya tuliyemuongeza kwenye kikosi chetu.
Kaze na Owino ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya URA ya Uganda wanatarajiwa kutambulishwa jumamosi katika mchezo wa kirafiki baina ya Simba na timu ya Taifa ya Polisi,mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ka