AZAM FC KUKIPIGA NA ORLANDO PIRATES AGOSTI 9


HABARI NA SOKA IN  BONGO BLOG
Washindi wa pili mfululizo wa ligi kuu ya Vodacom Azam Fc wanataraji kuelekea Afrika kusini kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu ya vodacom inayo tarajia kuanza agust 24 ambapo Azam Fc wataanzia mkoani Morogoro. 
Ziara hiyo ya maandalizi ya VPL yatajumuisha michezo minne ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kaizar Chief utakaochezwa Agost 5, dhidi ya Mamelodi Sundow utakaochezwa agusti 7, dhidi ya Orlando Pirates agust 9 na kuhitimisha Agust 12 dhidi ya Moroka Swalows. 
Azam FC itaondoka na kikosi kizima isipokuwa washambuliaji wa wili walio majeruhi ambao ni Humphrey Mieno na Brian Umonyi. 
 Wakati huo huo Azam Academy jana ilianza vyema mashindano maalum ya wiki ya kilimo mjini Kisumu baada ya kuifumua timu inayocheza KPL (Kenya Premier League) 1-0 goli likifungwa na Erick Haule katika dakika ya 60. 

Leo Azam FC watashuka tena uwanjani kukwaana na Chemeli Sugar FC ambayo nayo inacheza ligi kuu ya Kenya