ASHANTI UNITED YAPOTEZEA 'MKONO' WA YANGA SC, YAJIPANGA KUIADABISHA MGAMBO SHOOTING J5

LICHA ya kutandikwa mabao 5-1 na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, timu iliyopanda Ashanti United imesema haijakatishwa tamaa na kuanza kwao vibaya kwani hata mabingwa hao waliwahi kutandikwa mabao kama yao.
Msemaji wa timu hiyo Marijani amesema leo kwamba kufungwa ni sehemu ya mchezo hivyo wanajiopanga kwa ajili ya michezo mingine inayofuata.
Akienda mbali zaidi, msemami huyo alisema kwamba kipigo hiko hakitokani na ubovu wa timu yao bali ni ugeni walionao wachezaji wake ambao wengi wao wana umri mdogo tu.
"Kwa sasa tumetafuta mtaalamu wa saikoljia ili aweze kuwajenga wachezaji wetu ili waweze kucheza kikamilifu bila woga wowote,"alisema.
Akizungumzia mchezo wao unaofuta dhidi ya maafande wa Mgambo Shooting utakaopigwa jumatano , msemaji huyo alisema kikosi chao kimeshaewlekea jijini Tanga tayari kwa mchezo huo ambao anaamini utakuwa mgumu na uliojaa ushindani.
"Pamoja na yote tumejipanga kushinda licha ya kuwa mchezo wetu utakuwa mgumu kwani wapinzani wetu watataka kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wao uliopita,"alisema
Ikumbukukwe kuwa katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo, Mgambo ilitandikwa mabao 2-0 na maafande wwenzao JKT Ruvu katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani, Tanga.