ABDI KASSIM 'BABBI' ASAJILIWA KMKM

Aliyekuwa mchezaji wa Azam fc Abdi Kassim 'babbi' hatimaye amesajiliwa na klabu bingwa ya soka visiwani Zanzibar, KMKM.
Babbi ambaye mkataba wake na Azam ulimalizika msimu ulkiopita amethibitisha kujiunga na maafande hao kupitia ukurasa wake wa facebook hii leo.
"hi nyote ..nashukuru mungu mzima .wa afya ..nimesaini mkataba na kmkm mabingwa wa soka zanzibar na timu inayo shiriki mashindano ya kimataifa na mashindano mbali mbal ..ikiongozwa na coach mzoefu na mwenye ujuzi wa hali ya juu..ali bushir .so natowa shukrani dha dhati kwa uwongozi wa kmkm kwa kumaliza soezi la usajil kati yangu.na wao na napenda kuwashukuru wote wapenzi wa kmkm ..kwa kuniunga mkono bamoja na uwongozi wa juu na nafurahi zaid kwa vile nipo nyumbani ..na famly yangu na biashara zangu za hapa na pale..asanten sana..watanzania wote" .