YANGA YATANDIKWA 2-1 NA EXPRESS YA UGANDA

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Young Africans jana  imepoteza mchezo wake wa kirafiki kwa baada ya kufungwa mabao 2-1 na Express FC kutoka nchini Uganda katika mchezo uliofanyika katika daimba la uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Mchezo ulianza kwa kasi kwa timu zote kusaka bao la mapema lakini shuti la mshambulaji wa Yanga Shaban Kondo dakika ya ya nne ya mchezo lilipita sentimeta chache juu ya lango la timu ya Express.
Dakika ya 10 ya mchezo kiungo wa timu ya Express Mukasa Musa aliipatia timu yake bao la kwaza kufutia kuwatoka walinzi wa Yanga na kuachia kombora la mbali mita 25 ambalo lilijaa moja kwa moja langoni na kumshinda mlango Deogratius Munishi 'Dida'.
Yanga ilicheza vizuri sehemu ya kiungo na kutengeneza nafasi kadhaa, na katika dakika ya 30 ya mchezo, mpira uliorushwa na Mbuyu Twite ulimshinda mlinda mlango wa Express kabla ya Shaban Kondo kuugusa na Abdulhman Sembwan kuukwamisha wavuni na kuhesabu bao la kusawazisha.
Mpaka dakka 45 za kipindi cha kwanza, Young Africans 1 - 1 Express FC.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ambayo yaliongeza uhai na kasi ya mashabulizi lakini kutokua makini kwa washambuliaji kulifanya kukosa nafasi kadhaa za wazi na kukuta mashambulizi hayo yakiishia mikononi mwa mlinda mlango wa Express FC.
Dakika ya 77 ya mchezo nadoha wa Express FC Kavuma Willy aliipatia timu yake bao la pili akimalizia pasi safi iliyopigwa na Mukasa Musa kufuatia kumzidi ujanja mlinda mlango wa Yanga Dida na waganda hao kuhesabu bao la pili.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1 - 2 Express FC
Yanga: 1.Dida, 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Mbuyu Twite, 5.Rajab Zahir, 6.Bakari Masoud/Salum Telela, 7.Sospeter Mhina/Abdallah Mnguli, 8.Hamis Thabit/Nizar Khalfani, 9.Shaban Kondo/Jeson Tegete 10.Said Bahanuzi,Notikely Masasi, 11.Abdalhman Sembwana/Didier Kavumbagu .
CHANZO:www.youngafricans.co.tz

Comments