YANGA, SIMBA ZAKABIDHIWA VIFAA KWA AJILI YA MSIMU MPYA WA LIGI KUU BARA 2013/2014

Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe (Katikati) akionesha sehemu ya vifaa walivyokabidhi leo kwa klabu za Simba na Yanga kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2013/2014, kushoto ni Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala na Kulia ni Katibu Mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako

Ikiwa ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema “Tunawapatia vifaa mapema kabla ya ligi kuanza ili wapate muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2013/14 ambayo bila shaka itakuwa na changamoto kubwa kwa timu hizi mbili na pia tunaamini kuwa siri ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri. Ni matumaini yetu kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa Simba na Yanga wataiwakilisha Kili vizuri na kufurahia kuzichezea klabu hizi kongwe.”

Kavishe aliongeza kuwa Vifaa ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi, shin guards, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu.

Kilimanjaro Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.  

Kavishe alisema kuwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga umelenga kukuza soka la Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa.

Tunawashukuru viongozi wa Simba na Yanga, mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu.

“Tunawaomba mashabiki wa Simba na Yanga waendelee kuiunga mkono bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager kwani tunafanya kila jitihada kuwapa burudani na kufikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.”