YANGA, MTIBWA KUUMANA ALHAMIS MJINI TABORA

MABINGWA wa ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga Alhamis watashuka katika dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Tabora kuumana na Mtibwa Sugar ya Morogoro. 

Huo utakuwa mchezo wa tatu kwa Yanga ambayo ipo katika ziara ya kimichezo Kanda ya Ziwa baada ya Jumamosi  kutoka suluhu ya bao 1-1 na Express ya Uganda jijini Mwanza, kabla ya  kufungwa 2-1 na Express katika mechi ya marudiano iliyochezwa jana mjini Shinnyanga.