WASANII WAWAPONGEZA RAIS OBAMA, KIKWETE

Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umempongeza Rais wa Marekani,Barack Obama na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete kutambua mchango wa wasanii, wachezaji wa mpira hasa pale walipocheza ngoma na mpira wa miguu na mpira wa kikapu. 
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caasim Taalib alisema jana kuwa kitendo cha Rais Obama na mwenyeji wake Rais Kikwete kucheza ngoma za asili alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (DIA) imeonesha namna ambavyo wanaguswa na utamaduni wa mtanzania. 
Alisema pia kuwa hatua ya Rais Obama kutambua mchango wa mtanzania,Hasheem Thabit anayecheza mpira wa kikapu ligi ya NBA nchini Marekanikunaimanish anatambua Tanzania ilivyojaliwa na vipaji ndiyo maana mchezaji huyo amekuwa nyota kati ya waliosajiliwa kuchezea timu za
ligi hiyo. 
Taalib alisema ni faraja kubwa kuona Rais Obama kuonesha ufundi wake kumiliki mpira kwa kichwa na kumpasia Rais Kikwete alipotembelea mitambo ya kufua umeme ya Symbion ambayo ni mshirika wa Klabu ya Sunderland. 
‘SHIWATA baada ya kujua mchango wa Rais Obama iliahirisha Tamasha la Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga ili kutoa nafasi kwa  wasanii na viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya  Rais Obama’
 SHIWATA ambayo inaundwa na wasanii, wanamichezo, wanahabari na vijana wapatao 7,000 iliahirisha tamasha hilo na sasa litafanyika Agosti mwaka huu ambapo itakabidhi nyumba kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14
ambao wamekamilisha michango ya ujenzi  wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.
Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni mwanachama wa SHIWATA wangine ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
 Mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika eneo la hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili kujikwamua kimaisha.

Comments