STARS YAENDELEA KUWANOLEA MAKALI THE CRANES

Taifa Stars chini ya Kocha Kim Poulsen inaendelea kujinoa jijini Dar es Salaam tayari kuikabili Uganda (The Cranes) katika mechi ya kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Wazhezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) itakayochezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ratiba ya mazoezi kwa Taifa Stars ni kama ifuatavyo;
Jumanne- Julai 9 mwaka huu      Saa 9 alasiri        U/ Taifa
Jumatano- Julai 10 mwaka huu   Saa 9 alasiri        U/Taifa
Alhamisi- Julai 11 mwaka huu         Mapumziko
Ijumaa- Julai 12 mwaka huu       Saa 10 jioni         U/Taifa

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)