SIMBA KUKIPIGA NA URA JULAI 20 TAIFA

KLABU ya Simba inatarajiwa kuwatambulisha rasmi nyota wake wapya  iliyowasajili kupitia mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda utakaopigwa Julai 20 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Simba  kwa sasa ipo mkoani Katavi ilipokwenda kwenye ziara maalum ya kimichezo baada ya kualikwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambapo kabla ya kwenda huko ilianzia mkoani Tabora .
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala alisema jana kwamba maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanakwenda vema ambapo URA inatarajiwa kuwasili nchini Jumatano ijayo.
Alisema pamoja na mchezo huo kutambulisha wachezaji, pia utakuwa ni sehemu ya kukipima kikosi chake ambacho kipo katika maandalizi ya michezo yake ya msimu mpya wa Ligi Kuu soka tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu.
“Kama mjuavyo makocha wetu kwa sasa wanaendelea kukinoa kikosi hivyo kupitia mchezo huo watapata picha halisi ya kuona kasoro zilizopo katika kikosi na kuzifanya marekebisho,”alisema.
Mpaka sasa Simba imewasajili mshambulijiaji  Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa Sugar , Kipa Andrew  Ntalla kutoka Kagera Sugar, Beki Adeyum Saleh aliyekuwa anakipiga  Miembeni ya Zanzibar, kiungo Twaha Shekue ‘Messi’ kutoka Coastal union ya Tanga, Zahoro Pazi  kutoka JKT Ruvu akicheza kwa mkoppo kutoka Azam FC

 Aidha, Simba ina wachezaji wa kimataifa ambao baadhi yao wanawaniwa kusajiliwa wakiwemo James Kone wa Al  Nasri Juba ya Sudan Kusin, beki Mganda Asuman Buyinza  aliyekuwa anacheza soka la kulipwa nchini Sudan, Tambwe Asuman kutoka Vital’ O ya Burundi, Sammue Ssenkoon kutoka URA ya Uganda.